DiscoverChangu Chako, Chako Changu
Changu Chako, Chako Changu
Claim Ownership

Changu Chako, Chako Changu

Author: RFI Kiswahili

Subscribed: 10Played: 2,934
Share

Description

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

169 Episodes
Reverse
Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.
Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Msimamizi wa kituo cha radio China Kimataifa ambaye ni raia wa China kufahamu zaidi kwanini alivutiwa na swala la kujifunza lugha ya kiswahili, ni katika muktada wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania. Kwenye Muziki utasikiliza wimbo wa mwanamuziki Lupman mwenye asili ya Burundi anaefanya kazi yake huko Sweeden. https://www.youtube.com/watch%3Fv%3DdsIZZ0MmadE
Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambyo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Kongomano la nne la idhaa za Kiswahili duniani. Kwenye le Parler francophone nitakueleza ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Idd Aziz kutoka nchini Kenya.
Makala haya yameandaliwa na Florence Kiwuwa kwa ushirikiano na Ruben Lukumbuka.
Makala maalum ya changu chako chako changu inafanyika hapa Mombasa pwani ya Kenya katika luktadha wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kifaransa, inayofahamika Kama La Francophonie, ambapo Taasisi inayofundisha watu lugha hii na tamaduni za Ufaransa, Alliance Francaise ya Mombasa, imeandaa maadhimisho haya maalum kwa kuenzi namna ambavyo Francophonie inavyotia fora nchini DRC. Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka moja kwa moja akiwa Alliance francaise ya Mombasa
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na mwanaharakati Florence Kiwuwa ambae pia ni mtangazaji wa RFI Kiswahili kuhusu maandalizi ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani.
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu umuhimu wa kujifunza lugha Mama, wakati huu shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni Unesco likiwa na wasiwasi wa kutokewa kwa zaidi ya lugha mama zaidi ya 3000.
Makala haya ni sehemu ya pili ya historia ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika CAN.
Karibu kuungana naye Ali Bilali katika Makala ya leo Changu chako chako changu, ambapo anakuletea historia ya kombe la mataifa ya afrika na atiba ya shughuli kutoka Alliance francaise za ukanda na kwenye muziki atakuletea historia fupi ya mwanamuziki rapa kutoka nchini Kenya King Kaka. Kumbuka pia kumfolow kwa instagram @billy_bilali
Habari za asubuhi msikilizaji wa RFI Kiswahili na mpenzi wa Makala Changu Chako Chako changu, makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler franxophone na Muziki ambapo leo nimekuandalia Historia na utamaduni wa watu wa kabila la Wanyamwezi, nitakuletea pia mwanamukuzi Miraculos kutoka nchini Burundi Mimi naitwa Ali Bilali mtangazaji asiependa makuu. Karibu ama bienvenue. Usikosi pia kumfollow @billy_bilali
Katika Makala haya, mwanahabari wako Ali Bilali anarejelea historia ya mwanaharakati mtetezi wa Uhuru wa DRC Emery Patrice Lumumba aliezaliwa Julay 2 1925 alifariki Januari 17 mwaka 1961. Usikosi pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali
Makala haya Changu chako Chako Changu, Ali Bilali mtangazaji wako asipenda makuu amezungumza na Mzee Ebengela Saleh kuotka huko mashariki mwa DRC kuzungumzia kuhusu Historia na Tamaduni za watu wa Kabila la Wabembe. Utapata pia kumfahamu mwanamuziki kutoka Ufaransa mwenye asili ya DRC na Congo Brazaville Naza. Ambatana na mtangazaji wako na usikosi kumfollow kwa Instagram kwa kubonyeza hapa. @billy_bilali https://www.instagram.com/billy_bilali/
Katika Makala haya Ali Bilali anazungumzia kuhusu siku ya kuwambuka watu waliotoa mchango wao katika harakati za ukombozi ambapo kila januari 4 ni siku ya kuwakumbuka wapambanaji hao waliochangia katika ukombozi wa nchi Usikosi pia kumfollow mwanahabari wako Ali Bilali kwa Instagram @billy_bilali
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na vijana wanafunzi na waalimu wa lugha ya kifaransa kuangazia utamaduni wa kujifunza lugha hususan lugha ya Kifaransa, wakati kwenye kipengele cha Muziki amempokea mwanamuziki kutoka nchini Burundi Mistachampagne ambae anazuri jiji la Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki. Usikosi pia kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_bilali
Makala haya ni mkusanyko wa Makala za mwaka 2023 alizokukusanyia mtangazaji wako Ali Bilali
Katika Makala haya,Florence Kiwuwa mtangazaji wa maswala ya Historia na utamaduni kutoka RFI Kiswahili anakuletea historia ya wadigo wa Kenya na Tanzania  na kwenye le Parler francophone tutaangazia kuhusu maonyesho yake Dj Click katika ukumbi wa  Alliance Francaise ya Arusha nchini Tanzania. Na kwenye Muziki tutamuangazia mwanamuziki Koffi Olomide kutokea DRC.
Ni furaha kubwa kukutana nawe kwa mara nyingine tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo leo nitaungana na mwenzangu DENISE MAYO kukujuza kuhusu tamaduni za watu wa huko Katanga katika uchimbaji wa madini, kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba wa Alliance francaise za Ukanda na Institut Français ya Lubumbashi, kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Kutoka nchini Kenya Mohammed Ali Said, anaefahamika sana kama Masauti. Mimi ni Ali Bilali
Karibu mpenzi msikilizaji katika Makala ya leo Changu Chako Chako Changu, ambapo nakukumbusha historia na tamaduni ya watu wa kabila la wataita, na kwenye le parler francophone tutaangazia ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance France Francaise ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, na Institut francais ya Lubumbashi. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Hiro Le Coq rapa wa Ufaransa mwenye asili ya DRC. Mimi naitwa Ali Bilali bienvenue.
loading
Comments 
Download from Google Play
Download from App Store