DiscoverSiasa na Gumzo
Siasa na Gumzo
Claim Ownership

Siasa na Gumzo

Author: Standard Media

Subscribed: 0Played: 0
Share

Description

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
43 Episodes
Reverse
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha kutoka Marekani kupiga jeki Hazina ya Hustler Fund. Umesaidika na fedha hizo? Kiwango ulichoomba kimeongezeka? Pia kuna masaibu ya Cherera4. Unasemaje kuwahusu? Tribunal iendelee kuwachunguza au unasema leave them alone jinsi anavyotaka Baba? Wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi.
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu ya Tinga Kenya Kwanza, Tinga naye anasema wewe kijana wacha kuniota kila saa mimi si rika lako. Unamshauri vipi Riggy G? Vilevile Baba anataka Waluke kuachiliwa huru. Eti kesi dhidi yake itupiliwe mbali kama za wengine. Unasemaje? Kuhusu njaa, unadhani serikali imeweka juhudi za kutosha kukabili makali ya njaa? Alhamisi serikali ya Kenya ilituma msaada wa chakula Somalia ilhali hapa Kenya watu, mifugo wanaangamia. Kwa mengi wanahabari wetu Collins Chungani akiwa Nyeri, Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki Gumzo na Wakenya.
GMO imezua gumzo, Azimio wakipinga. Kalonzo naye anasema Rais Ruto analenga kuangamiza kilimo cha mimea ya kiasili. Mbali na hayo, unadhani kwamba Kalonzo anatoshea viatu vya Odinga katika upinzani? Baba naye angali anamlaumu Chebukati na mataifa ya kigeni, kwamba yaliingilia uchaguzi wa Kenya! Unasemaje? Si hayo tu, Azimio inasema Ruto amekuwa kiguu na njia, bila kwanza kutimiza ahadi kwa Wakenya. Nawe unatathmini vipi utendakazi wa Ruto ndani ya siku 30 tangu kuapishwa? Wanahabari wetu William Omasire wa Nyamira, Edwin Mbugua wa Nyeri, Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanasema na wananchi.
Mgombea urais wa UDA, William Ruto amezindua manifesto yake akiangazia nguzo sita; kupunguza gharama ya maisha, kumaliza uhaba wa walimu, matibabu bila malipo, kujenga nyumba elfu 250 kila mwaka, kukuza biashara na kuimarisha kilimo. Ahadi hizi zinatekeleka? Upande mwingine Wajackoyah ameweka wazi manifesto yake akijumuisha mambo ya kiajabu. Mara atahamisha jiji la Nairobi hadi Isiolo, sijui kufuga nyoka, kuvunja sekta ya bodaboda na kuwaajiri wahudumu hao katika mashamba ya bangi na mengine mengi ya kushangaza. Ni manifesto gani ni nzuri? Halafu Kenya Kwanza inasema bandari ya Mombasa imeuzwa huku serikali ikikana. Kadhalika Baba ameanza vita dhidi ya Chebukati. Anasema manual register sharti itumike sambamba na electronic. Chebukati anasema la hasha. Kwa nini Baba anasisitiza ni lazima manual itumike? Haya yanajiri huku suala la zoning likitikisa nyumba ya Baba. Wagombea wasio maarufu wanaambiwa wajiondoe kuwapisha wenye nguvu. Benard Lusigi wa Kakamega, Edwin Mbugua wa Nyeri na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.
Nyumba ya Kenya Kwanza imeanza kuwaka moto. Kuria na Kabogo wataka mkutano wa dharura wakimshtumu Gachagua kufuatia madai ya udikteta. Aidha, wanadai wana-UDA wanapendelewa katika kampeni za Kenya Kwanza. Kunani? Gachagua amekuwa mzigo Kenya Kwanza? Anavutia kura au anafukuza? Sakata ya Sakaja kuhusu digrii nayo yamfikia Tinga na Hustler. Kelele zimechacha kuhusu kisomo cha Tinga na PHD ya Hustler. Baba awataje classmates wake. Bei za mafuta zimeendelea kupanda. Tuwalaumu nani? Wanahabari wetu Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia sehemu hii.
Bunge la 12 limevunjwa rasmi baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Je, limetimiza matarajio ya Wakenya ama limekuwa bunge la demokrasia ama utumbokrasia kwa kujali tu donge nono kupitia marupurupu? Kura za maoni nazo zinaendelea kutolewa kuelekea uchaguzi mkuu. Je, ni za kuaminika ama zinatoa taswira ya kila mwamba ngoma kuvutia kwake? Raila Odinga naye ametangaza manifesto ambayo imeibua gumzo kuu hasa kwa kuzitaja nguo za mitumba kuwa za wafu yaani marehemu. Je, alieleweka visivyo? Wanahabari wetu, Martin Ndiema wa Trans Nzoia, Clintone Ambujo wa Kisumu na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wanatupambia gumzo la wiki hii tukianza na Kiraese.
Wasifu wa Hayati Stanly Emilio Mwai Kibaki aliyeongoza Kenya kati ya 2002 - 2012 na kuaga dunia tarehe 22/04/ 2022. Wasifu huu umeandaliwa na kusimuliwa na Victor Mulama.
Mchujo wa vyama vya kisiasa unapoendelea, lipo jambo moja bainifu kuhusu matokeo kuhusu ngome za Naibu wa Rais William Ruto kulinganishwa na ngome ya Raila Odinga. Kwenye eneo la Bonde la Ufa ambako Ruto ana ufuasi mkubwa, baadhi ya wanasiasa wenye tajriba wamelambishwa sakafu huku vijana wengi wakiingia ulingoni. Na huko Nyanza, wanasiasa wengi waliokuwapo uongozini wamedumishwa hasa katika nyadhifa za ubunge, useneta na ugavana. Aidha, katika ngome zote mbili, idadi kubwa ya wawakilishi wadi waliokuwapo wamelambishwa sakafu na wapya kushinda tiketi. Hali hii inamaanisha nini kisiasa? Beatrice Maganga analiangazia suala hili.
Uchaguzi mkuu unapokaribia kila chama cha kisiasa kinaweka mikakati ya kuhakikisha mchujo utaofanyika katika chama unakuwa huru na wa haki. Mkurugenzi Mkuu katika Chama cha UDA, Odanga Pesa vilevile Cathrene Muma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi ya ODM wanazungumzia mikakati mbalimbali inayofanywa na vyama vyao kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Baada ya kimya kingi na fukuzafukuza chamani, hatimaye Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi wa Jubilee katika Ikulu. Ikumbukwe chama hicho kimepanga Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe, NDC tarehe 25 Februari, 2022 katika Ukumbi wa KICC, mjadala ukiwa kuwafurusha rasmi Ruto na wandani wake kutoka chama hicho, mpango wa kushirikiana na miungano mingine na kumfanyia kampeni Raila Odinga. Vilevile mjadala mkali umechacha kuhusu mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi. Wana-OKA nao baada ya pigo la kondokewa na Musalia Mudavadi na Moses Wetangula imewapata washirika wengine wawili. Je, ni muungano gani una ufuasi makubwa? Kwa masuala na maswali haya, wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, Faith Kutere wa Uasin Gishu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wamewashirikisha wakazi katika gumzo wiki hii.
Katika Ukweli wa Mambo leo, tunaangazia hotuba ya Musalia Mudavadi wakati Kongamano la Kitaifa la ANC, Januari 23 mwaka wa 2022. Je, aliyoyasema yana ukweli ama la na kwa kiwango gani? Huu hapa ukweli wa mambo baada ya utafiti wa kina baina ya Shirika la Habari la Standard kwa ushirikiano na kampuni ya Africa Check. Katika hotuba yake ya kipekee ya kukubali uteuzi wa kupeperusha bendera ya urais kupitia chama chake, Musalia aliahidi kufufua uchumi jinsi alivyofanya alipokuwa Waziri wa Fedha miaka ya 90. Geoffrey Mung’ou anasimulia.
Mjadala mkali umetawala vinywa vya wengi wiki hii, kufuatia hatua ya Mudavadi na Wetangula kujiondoa katika OKA na kuungana na Ruto. Hatua hiyo imechochea gumzo huku wengi wakijiuliza je, Ruto atavuna kura nyingi za Magharibi dhidi ya Raila? Hatima ya Kalonzo katika OKA ni gani hasa? Atawania urais, ama ataungana na Raila katika Azimio la Umoja? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanaangazia makala hapa.
Earthquake aliyoahidi Musalia Mudavadi inasubiriwa kwa hamu kuu Jumapili. Amewaalika wana'OKA na kuwafungia nje Ruto na Raila. Wakenya wana maoni gani? Aidha, cheche baina ya Raila na Ruto zimezidi, kuhusu urushaji mawe na kuitana majina. Haya yanahatarisha utangamano nchini? UDA tayari imeandikia ICC ikidai serikali inafadhili vurugu kwa manufaa ya Raila. Vilevile tunaangazia kesi ya BBI katika Mahakama ya Juu. Je, reggae itarejea? Kadhalika tunazamia suala la mili katika Mto Yala. Wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na John Mbuthia wa Nyeri wanatupambia makala haya
Benson Cheserek ni miongoni mwa Wakenya ambao wanaishi ughaibuni (Kenyans in diaspora) na sasa analenga kuwania kiti cha ubunge kwenye eneo la Marakwet Magharibi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Cheserek amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 17 ambapo amefanya kazi katika jeshi la Marekani kwa miaka 8 kabla ya kuanza biashara yake binafsi. Kwenye mahojiano na mwanahabari Faith Kutere, Cheserek anasema analenga kutumia ujuzi wake katika idara ya usalama kusaidia kukabili ukosefu wa usalama kwenye Bonde la Kerio, kubadili maisha ya wakazi wa eneo la Marakwet Magharibi kupitia masomo miongoni mwa masuala mengine.
Wanasiasa kadhaa wamekamatwa kwa kuhusishwa na matamshi ya uchochezi. Swali ni je, kuna mapendeleo jinsi UDA inavyodai? Je, ni kamatakamata kwa kigezo cha mirengo ili kuleta usawa wa kisiasa? Aidha, Rais Kenyatta alifanya mkutano katika Ikulu na viongozi wanaounga mkono Azimio la Umoja akiwamo Raila ambapo wote walipigia debe Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa. Vigogo wa OKA walisusia mkutano huo wa Ikulu, licha ya kualikwa. Je, hatua yao inatoa picha gani?Vilevile, inadaiwa kwamba huenda Mudavadi akajiunga na Ruto, na Kalonzo kujiunga na Raila. Ikitokea hivyo, utapande gani utakuwa na nguvu? Masuala haya na mengine ndiyo yanayolipamba Gumzo la Maisha likiletwa kwako na wanahabari wetu, John Mbuthia akiwa Nyeri, Rose Mukonyo wa Machakos na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi.
Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa umekuwa kichocheo cha mjadala wiki hii, ambapo wengi wanajiuliza iwapo kufaulu kwake kutakuwa mwanzo wa wanasiasa kuaminiana. Je, iwapo mswada huo utafanywa sheria, tutarajie miungano gani, hasa kati ya nani na nani? Na je, mswada huu umeashiria upande gani kuwa na ubabe bungeni? Aidha, tunaangazia mwaliko wa Ruto kwa kina Mudavadi na Wetangula licha ya kusema hawajaalikwa wala kukutana na yeyote kujadili miungano. Je, kuna karata gani ambayo inachezwa na wanasiasa hawa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu. Vilevile mjadala kuhusu haja ya wanafunzi kufanyiwa vipimo vya kubaini iwapo wanatumia dawa za kulevya au la kabla ya kurejea shuleni. Je, unafikiri hatua hii itasaidia kudumisha nidhamu shuleni? Wanahabari wetu Faith Kutere wa Eldoret, Bernard Lusigi wa Kakamega na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wameshiriki gumzo na wananchi kuhusu masuala haya.
Mjadala mkali unaendelea kufuatia hatua ya Raila Odinga kuwatafuta marafiki wapya wa kisiasa, hasa kwenye eneo la Magharibi baada ya Mudavadi kusisitiza kwamba hatamuunga mkono tena. Aidha, Ruto anawataka Mudavadi na Wetangula wajiunge naye katika UDA. Si hayo tu, ipo hofu kutokana na kupanda kwa maambukizi ya korona hasa baada ya kugunduliwa kwa Omicron hapa Kenya. Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo yao kuhusu masuala haya.
Tangazo la Odinga kuwania urais kwa mara ya tano, ni ithibati kamili kwamba kinyang'anyiro kitakuwa kati yake na William Ruto. Je, hatima ya Kalonzo, Mudavadi na Wetangula ambao walikosa kufika Kasarani ni ipi? Aidha, Wakfu wa Mlima Kenya Foundation, MKFumesema Raila tosha. Je, unadhani wafanyabiashara hao wataamua mwelekeo wa siasa za Mlima Kenya ama ni wananchi ndio watakaoamua jinsi anavyosisitiza William Ruto? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo yao.
Kauli ya Rais Kenyatta kuwa Kenya ni namba sita barani Afrika kwa utajiri imewaghadhabisha Wakenya wanaosema umaskini umekithiri nchini. Kuhusu siasa, Rais Kenyatta anasema wanasiasa viana watashindwa na wazee licha ya mbio zao za kisiasa. Je, sasa ni wazi kuwa Uhur anamuunga mkono Odinga kuwania urais? Je, hatima ya OKA ni gani? Aidha, IEBC imejiondoa katika kamati ya pamoja ya maandalizi ya uchaguzi. Maoni yako ni gani? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraise wa Pokot Magharibi wametangamana na wananchi kuhusu masuala haya.
Naibu wa Rais William Ruto abebeshwa lawama kuhusu vuruga za Kondele. Je, vuruguzu hizo zilichochewa kisiasa anavyodai? Na je, Ruto alifanya makosa kumshtumu Odinga katika ngome yake? Adha, Wakenya wanahisi kwamba Kalonzo Musyoka amekosa mwelekeo na wakati umefika kwake kutangaza wazi msimamo wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Vilevile, Nick Mwendwa atakiwa kueleza jinsi amekuwa akiendesha shughuli za FKF. Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Washington Onyango wa Kisumu na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
loading
Comments 
loading
Download from Google Play
Download from App Store