Discover
Vijana na Mapenzi
41 Episodes
Reverse
Mitandao ya kijamii siku hizi imeanza kutumiwa na watu wengi kuwatafuta wachumba. Je, ni muda upi unaostahili kuchukua kabla ya kukutana ana kwa ana na mchumba wa mtandaoni? Tumewashirikisha wananchi katika gumzo hili wakiwamo vijana waliojaribu mapenzi ya mtandaoni vilevile mshauri kulihusu suala hili.
Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika. Tumezungumza na wananchi.
Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika.
Tumezungumza na wananchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, jamii imekuwa ikiyafanya kipaumbele maslahi ya mtoto wa kike baada ya kukandamizwa kwa miaka mingi. Wengi sasa wamepata nafasi ya kusoma na hata kuajiriwa. Lakini kuna wanaoamini kwamba mwanamke anapopata kazi na kuwa na cheo katika jamii, mara nyingi hujawa kiburi. Suala hili tunaliangazia kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile kupata ushauri kuhusu masuala ya ndoa.
Ulimwengu huu wa utandawazi umewapa wengi fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kuweka picha zao kujifurahisha na hata kuwafurahisha wengine. Kuna wale huweka picha wakiwa wamevalia nadhifu, wengine kujianika nusu uchi na kadhalika. Je, mwonekano wa mtu katika picha anazoweka mitandaoni unaweza kuchangia apate mchumba ama akose, hasa kwa wanaolenga kuwapata wachumba? Tumezunguma na wananchi kuihusu mada hii vilevile kupata wosia wa mshauri Bi. Rachel Mahungu.
Washauri wa masuala ya mapenzi watakweleza kwamba huwa ni kibarua kumtafuta mchumba na hasa mtu mtakayefaana maishani. Ili kumpata mpenzi ni lazima kwanza umtafute. Lakini je, ni mbinu zipi ambazo hutumiwa katika kutongoza? Msichana naye anaweza kufanya nini ili kumvutia mwanamume ambaye anampenda bila kutoa taswira kwamba ndiye anayemfukuzia mwanamume? Vijana na washauri wanatoa kauli zao kuihusu mada hii.
Katika siku za hivi karibuni yamekuwapo majaribio ya dawa za upangaji uzazi ambazo pia zinaweza kutumika miongoni mwa wanaume. Iwapo dawa hizo zitaanza kutumika, je, wanaume wanaweza kuaminika katika kuzimeza dawa hizo ama utakuwa mchezo wa paka na panya kati yao na wake zao? Tumezungumza na wananchi vilevile mshauri kulihusu suala hili.
Mwanamume anapokuwa mtu mzima, wengi hutarajia kwamba awe mwenye kujitegemea kimawazo na hata kuweza kujifanyia maamuzi ya busara. Hata hivyo, kuna wanaume ambao huitwa 'mamas boy' ambao hushtumiwa kwa kutojitegemea kimawazo na kuwasikiliza zaidi wazazi kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Je, ni sawa kwa mume kuzingatia zaidi ushauri wa mzazi badala ya mkewe?
Mwanamke anapopata mtoto nje ya ndoa ama kumzaa mtoto katika ndoa kisha kutengana na mumewe, wapo wanaojipata katika njia panda anapotafuta mchumba. Baadhi huhofia kuwa katika mapenzi kwa hofu ya kulaghaiwa tena na hofu ya kupata mwanamume atakayempenda pamoja na mwanawe. Je, mwanamke huyu afanye nini ili ampate mchumba wa kumwamini?Tunaliangazia suala hili kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Description. Wapenzi wanapokuwa katika mahusiano, mara nyingine huibuka hali za kutokuwa waaminifu. Katika kipindi hiki tuaangazia namna ya kumtambua mtu ambaye si mwaminifu kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Wapenzi huoneshana upendo wao kwa njia mbalimbali mfano kushikana mikono katika maeneo ya umma, kupigana pambaja na wengine kupigana mabusu hadharani. Lakini je, ni sawa kwa wapenzi kuandamana mara kwa mara mfano kwenye saloon, kinyozi na kadhalika ama hali hiyo huenda ikachangia kuzoeana sana kiasi cha kusambaratisha uhusiano? Tumewashirikisha wananchi kulihusu suala hili vilevile kupata kauli ya mshauri.
Ni msimu mwingine wa sherehe ya siku ya wapendanao tarehe 14 Februari. Siku hiyo hutumiwa na wapenzi wengi kuoneshana upendo. Baadhi hununuliana zawadi na hata kujitengea muda wa kufurahia mapenzi yao. Hata hivyo kwa wengine ni siku ya kawaida tu. Tunaangazia umuhimu wa siku hii na iwapo kuna ulazima wa kumpa zawadi umpendaye.
Mtu anapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi, mara nyingine hujipata katika hali ambapo analazimika kutengana na mpenzi wake. Kuna wale ambao husitisha kabisa mawasiliano kati yao huku wengine wakiyaendeleza licha ya kutengana. Je, ni sawa kuwasiliana na uliyetengana naye? Wananchi wanatoa kauli zao wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga. Aidha, washauri wawili, Rachel Mahungu na Malkia wa Vijembe wanatupambia podcast hii kwa ushauri nasaha.
Katika jamii, uhuru wa kutangamana huwafanya watu kuwa na marafiki, washirika wa kibiashara, kisiasa na kadhalika. Lakini je, inawezekana kwa mwanamume na mwanamke kuwa marafiki tu bila kuhusika kimapenzi, kwa kimombo inaitwa platonic friendship. Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili. Vilevile tuna hoja za mshauri.
Awamu hii ya Vijana na Mapenzi inaangazia kisa cha mwanadada ambaye licha ya kuolewa, hataki kwenda kuishi na mumewe na kupendelea aishi tu alikozoea kabla ya kuolewa. Anasema kwamba anakoishi, maisha ni rahisi kulinganisha na kwa mumewe. Tunaliangazia suala hili kwa kushirikisha kauli za wananchi na wataalam.
Kuna msemo kwamba pesa ni sabuni ya roho. Hata hivyo kuna wapenzi ambao hutengana licha ya kuwa na pesa nyingi na mtu kuamua kumwendea asiyekuwa nazo. Je, ni kipi kinachoweza kuchangia hali hii? Wananchi vilevile washauri wa masuala ya ndoa wanatoa kauli zao.
Kwa nini baadhi ya wanaume huwachumbia wake za watu wakijua fika kuwa wameolewa? Je, wa kulaumiwa ni nani? Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili vilevile ushauri wa mtaalam.
[09:19, 11/4/2021] Mungou: Mara nyingi watu wanapochumbiana, huwa kuna rafiki wa karibu anayeufahamu uhusiano huo. Hali hii huwafanya wengine kujipata katika hali ya kuanza kutongozwa na wapenzi wa marafiki zao. Iwapo utajipata katika hali hii, ni sawa kumfahamisha rafiki yako kwamba amdhaniaye ndiye kumbe siye?
Mara nyingi wapenzi hupenda kutia ladha katika mahusiano yao kwa kufanyiana mambo ambayo mtu hakutarajia. Kuna wale huenda kiasi cha kuwatembelea wapenzi wao bila kuwajulisha. Je, hatua hiyo inafaa ama ni lazima umjulishe mpenzi wako kwanza? Tumepata hisia za wananchi vilevile mtaalam wa masuala ya mahusiano kulihusu suala hili.
Ni jambo la kawaida wakati msichana anapoolewa aende kuishi na mumewe. Hata hivyo, kuna msichana anayesema yeye atabaki kwao kwani ni karibu na anakofanyia kazi na kukodi nyumba ya kuishi na mumewe ni gharama kwani anakofanyia kazi mume huyo ni mbali. Vijana wanatoa kauli zao huku mshauri, Rachel Mahungu akitumia utaalam wake kutoa ushauri kwa vijana























