DiscoverMazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Claim Ownership

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Author: RFI Kiswahili

Subscribed: 0Played: 0
Share

Description

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
130 Episodes
Reverse
Kulingana na jumuiya ya IGAD,  zaidi ya vifo 190 vimeriotiwa  katika eneo la pembe ya Afrika, huku watu wengine laki 7 wakiyahama makazi yao.
Sote tunataka familia zetu ziwe na chakula cha kutosha ili kula kile ambacho ni salama na chenye lishe. Na lengo la 2 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ni ulimwengu usio na njaa ifikapo 2030.  Lakini licha ya juhudi zinazowekwa, suala la njaa na uhaba wa chakula limeonyesha ongezeko la kutisha tangu 2015, hali hii ikichochewa na mseto wa mambo ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na upungufu wa uzalishaji wa chakula.Kisiwani Pate jimboni Lamu, hapa akina mama wana zaidi ya mashamba matatu ya pweza katika bahari hindi, kwa manufaa ya chakula na mapato. 
Wiki chache zilizopita, tulikuletea makala kuhusu pikipiki za umeme, na kupitia ukurasa wetu wa Facebook RFI KIswahili, tukawa na maswali mengi kuhusu pikipiki hizi. Katika makala haya tumemwalika, Raymond Kitunga, kutoka kampuni nyingine inayotengeneza pikipiki za umeme, Spiro Kenya, na hapa atakuwa anayajibu baadhi ya maswali kuhusu pikipiki hizi za umeme. 
Nchini Kenya, wakulima wameanza kukumbatia ukulima wa wadudu na hasa nzi aina ya black Soldier Fly, kama njia mbadala ya chakula cha mifugo wao.Kulingana na wanasayansi, nzi hawa wana proteni ya kiwanngo cha juu, na hivyo wanatoa nafasi bora kwa wakulima kuboresha vyakula vya mifugo yao.
Makala ya leo yaliandaliwa Florence Kiwuwa, yanaangazia juhudi za jamii katika mji wa Arusha nchini Tanzania, na kile wanachokifanya kupiga jeki harakati za kukabilianana taka za plastiki.
Mkutano wa COP28 uliafikia mataifa mbalimbali kuanza polepole kuachana na matumizi ya mafuta ya kisukuku, mataifa ya Afrika yakitoa wito wa mataifa yenye nguvu na yanayozalisha nishati hii kwa wingi kuwa mfano katika utekelezwaji wa hilo. Mwenyekiti wa shirika la vijana la Youth Survival Organization, YSO, linalojihusisha pia na mzingira, Humphrey Mrema kutoka nchini Tanzania, anaangazia jinsi mkutano wa COP28 ulivyokuwa na mambo yanayoweza kutekelezwa na nchi kufikia mwaka 2030 lakini pia mwaka 2050.
Suluhu za kiasili zinashirikisha hatua mbalimbali za kulinda na kurejesha mandhari ya bahari, maeneo ya maji na maeneo ya mijini ili viumbe hai waweze kukabiliana na changamoto kama vile usalama wa chakula na maji, mabadiliko ya hali ya hewa, hatari za maafa na afya ya binadamu. Suluhu hizi zinasaidia urejesho wa misitu, ardhioevu na pia kuabdili mbinu za kilimo zinazosaidia udongo wenye afya.Kuangazia suluhu hizi za kiasili katika mabadiliko ya hali ya hewa, tunaungana naye Fredrick Kihara, Mkurugenzi wa hazina ya maji Afrika katika shirika la The Nature Conservancy, TNC, nchini Kenya.
Mkutano wa mazingira wa kimataifa COP28 unaendelea jijini Dubai, Saudi Arabia, lengo lake likiwa ni kuangazia namna ya dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katika muktadha huo, mifumoikolojia ya bahari, ni nguzo muhimu katika kuisaidia dunia kuafikia lengo hili, kutokana na sababu kuwa bahari inasaidia kufyonza  asilimia 25 ya hewa ya kaboni.Hata hivyo, ongezeko la utoaji wa gesi hamijoto umeathiri pakubwa mifumoikolojia ya bahari zetu.Katika makala yetu hivi leo, tunatupia jicho namna jamii eneo la Pwani ya Kenya zinajihusisha na shughuli za urejesho wa mifumoikilojia ya matumbawe.
loading
Comments 
Download from Google Play
Download from App Store