DiscoverUchumi na Biashara
Uchumi na Biashara
Claim Ownership

Uchumi na Biashara

Author: Standard Media

Subscribed: 4Played: 2
Share

Description

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.
59 Episodes
Reverse
Baadhi ya kampuni za uagizaji na uuzaji wa magari nchini zimebadili mwelekeo na sasa zinajitosa katika uagizaji wa magari yanayotumia umeme. Kampuni ya hivi punde kufanya hivyo ni ya BasiGo na ya kwanza kuagiza mabasi 15 ya umeme ambayo yalitengenezwa na Kampuni ya BYD Automotive iliyo nchini Uchina. Mabasi haya tayari yamewasili nchini kupitia Bandari ya Mombasa na yanatarajiwa kutoa huduma za uchukuzi jijini Nairobi. Lakini je, mbona wafanyabiashara waanze kufuata muelekeo wa uagizaji wa magari ya umeme? Robert Menza amewahoji baadhi ya washikadau katika sekta hiyo
Huku msimu wa Krimasi na Mwaka Mpya ukikaribia Sekta ya Utalii inategemea sana msimu huu kuimarika kutokana na watalii wa mataifa ya kigeni wanaolenga kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii nchini. Mojawapo ya maeneo hayo ni eneo la Pwani hususani Kaunti ya Mombasa. Je, wafanyabiashara hasa wa hoteli za kitalii wamejiandaa vipi msimu huu? Robert Menza amezungumza na Josephat Iha ambaye ni Meneja wa Mauzo katika Mkahawa wa Massai Beach.
Licha ya serkali kuahidi kushughulikia changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo, bado mahangaiko yanashuhudiwa mwezi mmoja baada ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi. Wengi wa wafanyabiashara hao wanalalamikia kuongezwa kwa bei ya mafuta, na kusababisha hasara katika sekta ya matatu. Charles Macharia, mhudumu wa teksi na Jimmy Mwangi, mhudumu wa matatu wanatishia kugura biashara hii. Mwanahabari wetu Edwin Mbugua amefanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara hao katika Kaunti ya Nyeri.
Washikadau mbalimbali wanaunga mkono mpango wa ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu unaoendelezwa na serikali, mfano mradi wa Buxton Point katika Kaunti ya Mombasa unaoendelezwa na mfanyabiashara, Suleiman Shahbal na Serikali ya Kaunti ya Mombasa. Robert Menza amezungumza na Martin Kariuki, anayesimamia uuzaji wa nyumba hizo.
Licha ya Shirika la Afya Dunia, WHO kushauri kuwa binadamu anafaa kula mayai 180 kwa mwaka, imebainika kwamba taifa la Kenya halijaafikia kiasi hicho takwimu zikionesha kuwa mayai 36 tu huliwa kwa wastani kulinganishwa na mataifa mengine mfano taifa jirani la Uganda na Afrika Mashariki. Hali hii imesababishwa na Wakenya kuzalisha mayai kwa wingi kwa minajili ya kufanya biashara ikilinganishwa na Uganda ambapo huzalishwa vijijini. Mwanahabari wetu Martin Ndiema amesema na wafanyabiashara wa mayai kubaini jinsi uzalishaji na ulaji huathiri biashara yao.
Katika Makala Uchumi na Biashara Podcast, mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia, Martin Ndiema amesema na wakulima ili kubaini ikiwa wameridhia kupanda mimea iliyoboreshwa kwa njia ya kijenetiki yaani GMO. Wapo ambao wamekumbatia na wengine kuirai serikali kuutafakari upya kuhusu uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri wa kupitisha GMO. Aidha, amesema na mtaalamu wa mimea akizamia ubora wa mazao ya mimea ya GMO, soko la kimataifa na usalama wa chakula kwa matumizi ya binadamu.
Leo kwenye Makala Uchumi na Biashara mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia, Martin Ndiema anaangazia juhudi zinazowekwa na viongozi wa matabaka mbalimbali Barani Afrika kufanikisha kuwapo kwa sarafu moja inayopendekezwa kuitwa AFRO. Aidha amezamia suala la kuafikia boda huru kustawisha uchumi wa bara hili.
Mfanyabiashara Jimmy Wanjigi sasa anapinga kwamba taifa lina deni la shilingi trilioni 8.47 jinsi ilivyochapishwa na Benki Kuu-CBK. Kulingana na Wanjigi, deni ni chini ya trilioni 3. Pia amedai fedha za mikopo ya ndani kwa ndani-domestic debts hazikutumika katika miradi ya serikali badala yake kuibwa.
Wasaga-nafaka mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia wanasema hawatakubali kuuza unga wa pakiti ya kilo 2 kwa shilingi 100 hadi serikali itakapowafidia. Mmoja wao kwa jina Robert Wanyonyi anasema kufikia sasa hakuna mikakati iliyowekwa kuhusu jinsi watakavyofidiwa na serikali. Anasema mkutano wa Jumatano katika Ikulu ulihudhuriwa na wachache, wengi wao wakiachwa nje. Hata hivyo, amekiri kwamba wateja wamekosa kununua unga wakishinikiza kuuziwa kwa shilingi 100. Katika mahojiano na Martin Ndiema, Wanyonyi anasema huenda wasaga-nafaka wakatapa hasara iwapo hawatafidiwa. Wakenya nao wanaipongeza serikali kwa kupunguza bei ya unga wa mahindi.
Wakenya wameendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, serikali nayo ikizidisha deni hadi trilioni 10 sasa. Aidha, wabunge na maseneta wamelaumiwa kwa kupitisha pendekezo la kuongeza deni la taifa kutoka shilingi trilioni 9, hadi 10 hali inayochangia kupanda kwa bei za bidhaa. Mike Ekutan ametangamana na Wakenya mjini Lodwar, Kaunti ya Turkana.
Bi. Mwansa, mwanamke mwenye umri wa miaka 70 amekuwa akijihusisha na upishi wa vyakula mbalimbali ambavyo huviuza kwa wateja kila siku, biashara ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka arubaini sasa. Biashara hii aliitegemea sana kuyakidhi mahitaji yake pamoja na wanawe kukiwamo kugharimia karo ya ya wanawe. Mwanamke huyu ambaye ni mkazi wa Majengo, Mvita katika Kaunti ya Mombasa anajihuisha na upishi wa chapati na maharagwe ya nazi. Vyakula vingine ambavyo pia Bi. Mwansa hupika ni mikate ya sinia na mitai. Kupanda kwa gharama ya bidhaa za upishi ukiwamo ya unga wa ngano, mafuta ya kupikia miongoni mwa bidhaa nyingine ambapo huzitumia kwa upishi kumemwathiri sana. Mwanahabari wetu wa Mombasa Robert Menza amezungumza naye katika Uchumi na Biashara Podcast
Wakenya wanaendelea kulalamikia ongezeko la bei za bidhaa ya kimsingi na kupanda kwa gharama ya maisha. Wengi wameamua kupunguza matumizi ya fedha kukiwamo kutembea badala ya kutumia magari au bodaboda na kula chakula mara moja kwa siku. Martin Ndiema amesema na Wakenya mjini Kitale.
Vincent Oduor akumbuka jinsi alivyoathiriwa na ghasia za baada ya uchaguzi, kazi yake ya ushonaji kutumia cherahani ikiathirika pakubwa. Anakumbukwa jinsi mashine za ushonaji zilivyoibwa wakati wa ghasia hizo. Kwa sasa kazi yake inanawiri na anapata faida
Uchumi wa Kenya uliimarika mwaka wa 2021 baada ya kuathirika kufuatia Janga la Korona mwaka wa 2020. Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Takwimu, KNBS uchumi ulikua kwa asilimia 7.5, kiwango hiki kikitajwa kuwa cha juu zaidi baada ya kipindi cha miaka kumi na mmoja. Aidha, nafasi 923,100 za kazi zilibuniwa katika mwaka huo wa 2021, wageni waliokuja nchini wakiongezeka hadi 871,300. Esther Kirong ametupambia makala haya.
Je, tangazo la Rais Kenyatta kuhusu asimilia 12 ya nyongeza ya mshahara wa chini kwa wafanyakazi, linamaanisha nini? Na je, ni wafanyakazi gani hasa watakanufaika kutokana na agizo hili ambalo limetakiwa kutekelezwa kuanzi mwezi huu? Jinsi anavyoarifu Victor Mulama, ni wafanyakazi wa viwango vya chini pekee ndio watakaoathirika, na licha ya hayo nyongeza ya mshahara itatozwa kodi.
Serikali ikijizatiti kufanikisha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa Wakenya, Kampuni ya ABC Homes vilevile imeweka mikakati kuhakikisha mpango huo unafaulu. Mhandisi Eveline Muringa ambaye ni Meneja wa Mradi wa ujenzi wa nyumba hizo anasema kwamba lengo lao hasa ni kuhakikisha Wakenya wengi wanamiliki nyumba kwa gharama ya chini. Robert Menza amezungumza naye.
Leo katika kitengo hiki tunaandazia mahangaiko ya waendeshaji pikipiki kufuatia msako katika harakati za kuinadhifisha sekta ya bodaboda. Msako huo ambao hata hivyo ulisitishwa kuruhusu mazungumzo, umesababisha madhara wahudumu hao wanaokiri ndoa zao zinayumba, wake zao wakiwatoroka kwa kutokuwa na fedha. Mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia , Martin Ndiema ametangamana na baadhi yao na kufanya mahojiano nao.
Wakenya kwenye maeneo yanayoendeshwa kilimo msimu huu wanalalamikia kupanda kwa bei ya mbolea kwa zaidi ya asilimia hamsini, huku mbolea gunia moja ya kilo hamsini ikiuzwa kwa shilingi elfu sita na hata elfu saba mia saba katika baadhi ya maduka. Wakulima wanadai kuwa bei ya mbolea ni ya juu sana ikilinganishwa na bei ya mahindi gunia moja la kilo tisini hivyo kupandisha maradufu gharama ya uzalishaji. Aidha, kuna wale ambao tayari wanasema kuwa hawataweza kupanda mahindi msimu huu kutokana na kupanda kwa gharama ya uzalishaji. Tumezungumza na mkulima Samuel Lelei Karuma.
Wahudumu wa bodaboda wamewalaumu polisi kwa kuwahangaisha wakitekeleza agizo la Rais kunadhifisha sekta hiyo. Kulingana Wycliffe Nyanamba, Mwenyekiti wa Wanabodaboda hapa jijini Nairobi, polisi wanawahangaisha hadi kwenye makazi yao wakiendesha msako huo wengine wakiwapunja pesa. Hata hivyo, Nyanamba amewalaumu baadhi ya wahudumu hao kwa kukiuka sheria za trafiki. Msako huu unafuatia kisa ambapo wanabodaboda wa Forest Road walimvamia na kumdhulumu kimapenzi mwanamke mmoja. Kauli yake inajiri wakati ambapo oparesheni hiyo imesitishwa kwa muda kupisha mazungumzo.
Patrick Wachira, mfanyabiashara wa kuyauza magari anasema amefanya biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ila korona ilimsababishia hasara ya mamilioni ya fedha. Kwa mujibu wa Wachira, biashara ya magari ni bahati nasibu kwani huwezi kujua idadi ya magari utakayouza kwa mwezi au wiki. Aidha, Wachiri amesema Wakenya hawajakumbatia magari ya umeme kikamilifu. Robert Menza amezungumza naye.
loading
Comments 
Download from Google Play
Download from App Store