DiscoverSBS Swahili - SBS Swahili
SBS Swahili - SBS Swahili
Claim Ownership

SBS Swahili - SBS Swahili

Author: SBS

Subscribed: 183Played: 10,315
Share

Description

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili
1243 Episodes
Reverse
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.
Waziri wa Shirikisho wa Mawasiliano amesema Optus inastahili tarajia adhabu kubwa, kufuatia kupotea kwa huduma ya namba ya dharura ya 000, hali ambayo ime husishwa na vifo kadhaa.
Taratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.
Kampuni ya pili kwa ukubwa ya madini imetangaza inapunguza ajira. Anglo American Australia imesema ita angaza kupunguza idadi ya wafanyakazi Queensland, na takriban wafanyakazi 200 wata athirika.
Maelfu ya watu wanasherehekea kuwa raia wapya wa Australia, katika sherehe zilizo andaliwa na halamshauri za jiji kote nchini kwa siku ya Uraia wa Australia.
Je, unajua jinsi ya kujigamba kuhusu gari lako?
Naibu Waziri Mkuu Richard Marles amekana madai kuwa uwekezaji wa $12 bilioni iliyo tangazwa juzi ime undwa ili kutuliza maombi ya Marekani kwa Australia kuongeza matumizi yake katika ulinzi.
Je, unajua jinsi ya kuelezea kuhusu anga la usiku?
Popote ulipo nchini Australia, kutoka jiji kuu lenye shughuli nyingi, hadi katika viunga vya mji, katika mji wa kikanda au kijijini, kuna uwezekano unaweza kutana na aina mbali mbali za wanyamapori wazuri wa Australia.
Benki ya ANZ imekiri kujihusisha na mwenendo usiofaa, katika huduma iliyotoa kwa serikali ya Australia, kulingana na Tume ya Uwekezaji na usalama ya Australia (ASIC).
Waziri wa Sheria wa zamani wa DR Congo, Constant Mutamba amehukumiwa na mahakama mjini Kinshana kufanya kazi ngumu kwa miaka mitatu.
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Félicien Kabuga anakabiliana na wakati mgumu kupata nchi itakayo mpokea kwa muda kutoka gereza la The Hague, Uholanzi.
Waziri Mkuu amesifu msaada wa wanachama wa kongamano la Visiwa vya Pasifiki, Australia inapo saka uenyeji wa kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa la, COP-31.
Je, unajua jinsi ya kuwapa watu mwaliko rasmi na usio rasmi?
Cervical cancer is preventable, but only if you catch it early. Cultural and personal barriers have often meant that women avoid cervical cancer testing. But now with the help of a world-leading test, Australia is aiming to eliminate cervical cancer by 2035. The test is a safe and culturally sensitive option for women from all backgrounds. Best of all it could save your life—or that of someone close to you. - Saratani ya Kizazi inaweza zuiliwa, kama ina gunduliwa mapema. Vizuizi vya kitamaduni na kibinafsi mara nyingi vime kuwa na maana kwamba, wanawake wanachelewesha kufanya uchunguzi wa saratani ya kizazi. Ila sasa, kwa msaada wa kipimo kinacho ongoza duniani, Australia ina lenga kutokomeza saratani ya kizazi kufikia mwaka wa 2035. Uchunguzi huo ni salama, na kitamaduni ni chaguo nyeti kwa wanawake kutoka mazingira yote. Muhimu zaidi, kipimo hicho kinaweza okoa maisha yako au mtu wa karibu yako.
Saratani ya Kizazi inaweza zuiliwa, kama ina gunduliwa mapema.
Dau Akouny, mmoja wa wavulana wawili walio uawa katika shambulizi la kisu mjini Melbourne wikiendi iliyopita, amekumbukwa na familia yake kama "mtoto mzuri" na alikuwa "sehemu ya mustakabali wa kesho wa jumuiya."
Serikali ya shirikisho imetangaza mpango wenye thamani ya $30 milioni, kupiga jeki idadi ya wakufunzi wa elimu ya ufundi.
Waziri wa mambo ya tamaduni nyingi Anne Aly, amechangia ujumbe wa mshikamano na jumuiya yawa Hindi wa Australia, kufuatia maandamano dhidi ya wahamiaji.
loading
Comments 
loading