DiscoverHabari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Author: United Nations

Subscribed: 133Played: 15,042
Share

Description

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
1246 Episodes
Reverse
Katika Siku hii ya Kimataifa ya Nishati Safi mwaka huu iliyobeba maudhui “Nishati safi kwa wote”, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia inaelekea kubadilika lakini ameonya kuwa kasi ya mabadiliko hayo kuelekea nishati safi haitoshi na ni lazima iongezwe. Flora Nducha na taarifa zaidi
Nchini Kenya, mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha uzalishaji wa nishati mbadala unaongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2030 unazidi kushika kasi kwani hivi sasa hata wavuvi na wamiliki wa migahawa wameanza kutumia majokofu yanayotumia nishati ya sola kuhifadhi samaki, na hivyo kuwa na sio tu uhakika wa samaki wakati wote bali pia wachuuzi kuepukana na kitoweo hicho kuoza umeme unapokatika. Assumpta Massoi anatupatia simulizi hiyo ya mafanikio kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati endelevu, IRENA.
26 JANUARI 2026

26 JANUARI 2026

2026-01-2611:20

Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kuelekea nishati safi, wavuvi nchini Kenya wanaotumia nishati safi kuhifadhi samaki yao kwa ajili ya kuuza, na mradi wa FAO wa masuala ya biashara HASTEN unaosaidia wajasiriamali nchini Rwanda.Katika Siku hii ya Kimataifa ya Nishati Safi mwaka huu iliyobeba maadhui “Nishati safi kwa wote”, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia inaelekea kubadilika lakini ameonya kuwa kasi ya mabadiliko hayo kuelekea nishati safi haitoshi na ni lazima iongezwe.Nchini Kenya, mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha uzalishaji wa nishati mbadala unaongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2030 unazidi kushika kasi kwani hivi sasa hata wavuvi na wamiliki wa migahawa wameanza kutumia majokofu yanayotumia nishati ya sola kuhifadhi samaki, na hivyo kuwa na sio tu uhakika wa samaki wakati wote bali pia wachuuzi kuepukana na kitoweo hicho kuoza umeme unapokatika. Assumpta Massoi anatupatia simulizi hiyo ya mafanikio kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati endelevu, IRENA.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo Duniani FAO, kupitia mradi wake wa masuala ya biashara HASTEN limeendesha warsha maalum ya kuanzisha biashara kwa vijana na wanawake,  mjini Kigali Rwanda, lengo likiwa ni kuwapa miradi 10 mipya ya biashara itakayofanyika kwa msaada maalum kutoka kwa wakufunzi wa kitaifa na kimataifa juu ya mbinu za kupanua biashara, kuongeza ufanisi na kuchangia katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula  na kilimo Duniani FAO, kupitia mradi wake wa masuala ya biashara HASTEN limeendesha warsha maalum ya kuanzisha biashara kwa vijana na wanawake,  mjini Kigali Rwanda, lengo likiwa ni kuwapa miradi 10 mipya ya biashara itakayofanyika kwa msaada maalum kutoka kwa wakufunzi wa kitaifa na kimataifa juu ya mbinu za kupanua biashara, kuongeza ufanisi na kuchangia katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Sheilah Jepng'etich na taarifa zaidi.
Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hii leo historia na dharura vilikutana chini ya paa moja. Ni miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC  lifanye kikao chake cha kwanza tarehe 23 Januari 1946 na linaadhimisha hatua hii muhimu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni wa maamuzi kwa mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa. Flora Nducha amefuatilia maadhimisho hayo na hii hapa taarifa yake
23 JANUARI 2026

23 JANUARI 2026

2026-01-2311:40

Hii leo jaridani tunaangazia miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, AI katika elimu na juhudi za kuhakikisha wananchi wamepata huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi nchini Niger.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hii leo historia na dharura vilikutana chini ya paa moja. Ni miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC lifanye kikao chake cha kwanza tarehe 23 Januari 1946 na linaadhimisha hatua hii muhimu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni wa maamuzi kwa mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa.Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya "SIKU ZA MUAMBO" katika muktadha wa uchumi.
22 JANUARI 2026

22 JANUARI 2026

2026-01-2211:26

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumsikia kijana Baraka Ayubu ambaye amekuwa kielelezo cha jinsi teknolojia inavyoweza kuleta mageuzi katika mifumo ya ujifunzaji na ustawi wa wanafunzi.Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa uchunguzi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaohusishwa na vita kati ya Hamas na Israel huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel utaendelea, licha ya kuanzishwa kwa Bodi ya Amani ya Gaza ambayo imezinduliwa hii leo na Rais wa Marekani Donald Trump.Tuelekee nchini Kenya ambako zaidi ya watu milioni mbili wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa uhakika wa kupata chakula kufuatia msimu wa mvua fupi za mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2025 kuwa mkavu zaidi kuwahi kurekodiwa. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, uhaba wa maji unalazimu familia kutegemea vyanzo visivyo salama, jambo linaloongeza hatari ya kipindupindu, homa ya matumbo, na magonjwa ya kuhara.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani, WHO, la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na la Makazi, UN-Habitat, kwa pamoja wamezindua mwongozo mpya unaozitaka serikali na viongozi wa miji kuweka kipaumbele kwa watoto katika upangaji wa miji ili kurejesha maeneo ya michezo yanayozidi kutoweka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya "SIKU ZA MUAMBO" katika muktadha wa uchumi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji kutokana na mvua zinazoendelea, serikali ya nchi hiyo ya kusinimashariki mwa Afrika imetangaza kuwa hadi kufikia sasa imerekodi vifo vya watu 120 na maelfu ya nyumba zimeharibiwa huku kiwango kikubwa cha fecha kikihitajika. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi  mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha. Sheilah Jepngetich na taaarifa zaidi.
21 JANUARI 2026

21 JANUARI 2026

2026-01-2110:45

Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji, ripoti inayomulika kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, na mradi unaolenga kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.Kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji kutokana na mvua zinazoendelea, serikali ya nchi hiyo ya kusinimashariki mwa Afrika imetangaza kuwa hadi kufikia sasa imerekodi vifo vya watu 120 na maelfu ya nyumba zimeharibiwa huku kiwango kikubwa cha fecha kikihitajika.Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU leo kimetoa ripoti ikitangaza kuingia kwa “enzi ya kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na mmomonyoko wa udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU  kimetoa ripoti inayotangaza kuingia katika“zama za kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kulikoni ?  Flora Nducha anaeleza kwa kina ripoti hiyo.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu ONNI SIGALA Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana ya neno “KING’ANI”
20 JANUARI 2026

20 JANUARI 2026

2026-01-2011:51

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako wasichana juhudi za kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) zimewezesha vijana wa kike kushiriki masomo ya Teknolojia ya Habari na Maewasiliano, TEHAMA na kujifunza stadi za teknolojia ili waweze kuedeleza biashara ya mtandaoni pamoja na matumizi mengine.Zaidi ya watu nusu milioni wameathiriwa na mafuriko makubwa katika mikoa ya kusini na kati ya Msumbiji, huku mvua kubwa ikiendelea kuvuruga usafiri, huduma za afya na njia za ugavi. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA nchini humo, Paola Emerson, amewaambia waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi kuwa majimbo ya Gaza, Sofala na Maputo ndiyo yaliyoathirika vibaya zaidi.Huko Mashariki ya Kati mapema leo Jumanne, vikosi vya Israel vimebomoa kwa tingatinga makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, huko Yerusalemu Mashariki eneo linalokaliwa kimabavu na Israel. Mkuu wa UNRWA, Philippe Lazzarini, amelieleza tukio hilo kama “shambulio lisilo na kifani dhidi ya Umoja wa Mataifa,”.Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, leo imesema imeanza kutekeleza mpango wa kurejesha kwa hatua mamlaka ya dola katika mji wa Uvira, mashariki mwa nchi hiyo, kufuatia kuondoka kwa kundi lenye silaha la AFC/M23. Serikali inasema vikosi vya usalama, polisi na huduma nyingine za serikali vinarejea ili kulinda raia, kulinda mali na kuleta utulivu katika eneo hilo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu ONNI SIGALA Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana ya neno “ KING’ANI”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, baada ya ziara yake ya siku tano nchini Sudan, ametahadharisha kuhusu kuongezeka kwa hali mbaya zaidi ya ukikukwaji wa haki za binadamu na ongezeko la janga la kibinadamu nchini humo.Rashid Malekela na taarifa zaidi.
Tathimini mpya iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imeonya kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa duniani mwaka 2025, ikisema kuwa idadi ndogo ya nchi ndiyo inachochea mwenendo huu unaotia wasiwasi kubwa wa haki za binadamu. Flora Nducha ameisoma tathimini hiyo na hapa anafafanua zaidi
19 JANUARI 2026

19 JANUARI 2026

2026-01-1911:28

Hii leo jaridani tunaangazia ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa duniani mwaka 2025, hali ya kibinadamu nchini Sudan na utafiti wa kutumia nyuklia kuwafanya tasa mbu dume nchini Austria.Tathimini mpya iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imeonya kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa duniani mwaka 2025, ikisema kuwa idadi ndogo ya nchi ndiyo inachochea mwenendo huu unaotia wasiwasi mkubwa wa haki za binadamu.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, baada ya ziara yake ya siku tano nchini Sudan, ametahadharisha kuhusu kuongezeka kwa hali mbaya zaidi ya ukikukwaji wa haki za binadamu na ongezeko la janga la kibinadamu nchini humo.Utafiti wa kutumia nyuklia kuwafanya tasa mbu dume ili kudhibiti magonjwa ya dengue, virusi vya zika na chikungunya nchini Austria umeonesha matumaini ya kupunguza mbu mwitu jike aina ya Aedes albopictus anayeeneza vimelea vya magonjwa hayo. Utafiti ulifanyika mwaka jana kwa ushirikiano kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la nishati ya atomiki, IAEA na la chakula na kilimo, FAO.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Utafiti wa kutumia nyuklia kuwafanya tasa mbu dume ili kudhibiti magonjwa ya dengue, virusi vya zika na chikungunya nchini Austria umeonesha matumaini ya kupunguza mbu mwitu jike aina ya Aedes albopictus anayeeneza vimelea vya magonjwa hayo. Utafiti ulifanyika mwaka jana kwa ushirikiano kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la nishati ya atomiki, IAEA na la  chakula na kilimo, FAO. Assumpta Massoi anaelezea zaidi.
loading
Comments (6)

Kelvin Zawadi

hongereni naamini siku moja wa Tanzania na East Africa kwa ujumla tuta anza kutumia podcasts kwa wingi

Feb 16th
Reply (5)