Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameapa kuchukua kila sehemu ya ardhi ya nchi yake iliyo chini ya udhibiti wa wapiganaji wa RSF, huku akikataa majadiliano yanayolenga kumaliza vita nchini humo.
Licha ya hatua zilizopigwa, walimu kwenye nchi nyingi za Afrika wanalipwa mishahara midogo na wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.Tunakuuliza je, walimu wanathaminiwa vya kutosha katika jamii yetu? Nchini mwako hali ikoje na nini kifanyike kuthamini na kuboresha maslahi ya walimu?
Kila siku ya Ijumaa tunakupa nafasi uzungumzie jambo ambalo umeliwazia wiki hii au pia habari kuu ulizozisikia katika matangazo yetu ya juma hili.