DiscoverMAELEZO PODCASTS
MAELEZO PODCASTS
Claim Ownership

MAELEZO PODCASTS

Author: Tanzania Information Services Department, Habari-MAELEZO

Subscribed: 22Played: 145
Share

Description

Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.

37 Episodes
Reverse
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mradi wa kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW). Mradi wa REGROW ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na lengo kuu la mradi huu ni kuboresha maeneo yenye vivutio vya utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.Hii ni pamoja na kuboresha usimamizi wa maliasili na kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ili kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya kiuchumi nchini . Serikali inadhamiria mradi huu uwe wa mfano katika kuleta maendeleo kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa na Waandishi wa Habari mkoani Singida, Septemba 26, 2021 #Kaziiendelee
Tuache Upotoshaji!

Tuache Upotoshaji!

2021-08-0303:41

Maelezo ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO juu ya Upotoshaji unaoendelea mitandaoni kuhusu Chanjo ya UVIKO-19
Hayasahauliki

Hayasahauliki

2021-03-2207:03

Wimbo huu ni zawadi kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. JPM  alikua baba wa wanyonge, mtetezi wa masikini na mzalendo wa kweli. JPM anaishi na ataishi ndani yetu milele.
UHURU, Sikiliza hapa!

UHURU, Sikiliza hapa!

2020-12-0519:46

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma.  Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa
Watanzania kwa ujumla tuanze kupanda miche ya kisasa ya Michikichi kutokana  na nchi kutumia gharama kubwa kuagiza mafuta ya mawese yatokanayo na zao hilo kutoka mataifa mengine duniani.
Hili nalo litapita!

Hili nalo litapita!

2020-05-1504:16

loading
Comments