Discover
NTAMWETE EMPIRE

8 Episodes
Reverse
Karibu kwenye uchambuzi wa mechi za NBC Premier league kwa wiki ya 13.
Baada ya mashindano ya kombe la mapinduzi kumalizika leo tunakuletea tathimini ya fainali hiyo na baada ya Clatous Chama kurejea Msimbazi tutaangalia umuhimu wake kikosini hapo na kitu gani anaweza kuongeza kwa timu iliyopo sasa.
Kesho ndio mashindano ya mapinduzi cup yanafika tamati ambapo tutashuhudia mchezo wa fainali utakaozikutanisha Azam FC dhidi ya Simba SC huko visiwani Zanzibar.Hapa NTAMWETE EMPIRE tunakuletea tathimini ya mchezo huo na nani mwenye nafasi kubwa kuibuka na ushindi na kwa sababu zipi, karibu.
Karibu kwenye makala maalum ya mashindano ya AFCON na MAPINDUZI CUP tukiangalizia kimbinu timu zilizofanikiwa kwenye mshindano hayo mpaka sasa.
Makala ya 31 ya mashindano ya soka ya mataifa ya Afrika inaanza jumapili hii ya Januari 9, leo tunaangazia timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Makala ya michezo ya kombe la mataifa barani Afrika AFCON inatarijiwa kuanza Januari 9,2022.Licha ya kuzongwa na kupigwa vita na baadhi ya watu hasa wanahabari toka barani ulaya, kuanzia leo tutakuwa tukikuletea mfululizo wa matukio na matokeo ya michezo mbalimbali tolavpale Cameroon, kaa tayari kwa uchambuzi uliotukuka kutoka kwa Dokta wa uchambuzi Bw. SHABELE DANIEL hapa hapa Ntamwete Empire.
Makundi ya klabu shiriki kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika tayari yamepangwa na wawakilishi pekee ya Tanzania kwenye mashindano hayo Simba SC wamepangwa kundi D pamoja na Gendarmerie ya Niger, Asec Mimosas ya Ivory Coast pamoja na RS Berkane ya Morocco.Ni jambo gani lifanyike ili Simba SC waweze kufika hatua ya Robo Finali?
Maeneo ambayo Simba SC na Yanga SC wanapaswa kufanyia kazi.




