PHONECALL PODCAST

Podcast ya dakika 60 ipo based on twitter ambapo inafanyika interview kwa njia ya simu ya mkononi ambapo yanaulizwa maswali tofauti tofauti kwa mmoja wa watu ambae atabahatika kupigiwa simu siku ya Ijumaa. Katika Phone call fotty ataongea na Influencers,wafanyabiashara,wasanii na watu wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii.

S04EP02 with Lucas Malembo 🚜

Kila mtu ana story yake kwenye maisha na haijalishi ni wakati mgumu kiasi gani unapitia kwenye maisha yako tambua kila mtu anapitia magumu yake. Lucas Malembo ni mwanzilishi wa "Malembo Farm" inayojishughulisha na maswala yote ya kilimo, Malembo ana amini kua kilimo kinaweza kutengeneza ajira kwa vijana wengi na vile vile kuikuza nchi yetu ki uchumi. Wengi tumemzoea Lucas Malembo akiongelea kilimo mara kwa mara ila kwenye episode hii amegusia mambo aliyopitia kwenye maisha yake kupelekea kuzaliwa kwa "Malembo Farm". Ni matumaini yangu utafurahia mahojiano haya na kujifunza mambo mengi

10-21
01:24:28

S04EP01 with BIG 👶🏽

Kwenye maisha ya kila siku watu napitia mambo mengi ikiwemo kutafuta hela, stress za familia, stress za kazi n.k na mitandao inabidi iwe sehemu ya mtu kupata furaha hata kama siku yake ilikua mbaya kiasi gani. Kupitia mtandao wa twitter kuna kijana anaitwa "Big0047" yeye huwa anatengeneza memes kwa njia ya picha na watu wengi wamekua wakifurahishwa na ubunifu wake. Tumeongea kuhusu mtandao uliompa yeye umaarafu na story nyingine kibao kumuhusu yeye. Natumaini utaenjoy mahojiano haya.

10-14
58:12

S03EP08 with Joyce Kiango📝

Mwalimu ni mtu muhimu sana kwenye maisha yetu na walimu wamebadilisha maisha ya watu wengi sana. Leo nimefanya mahojiano na mwalimu wa watoto wadogo ambae amejichukulia umaarufu mkubwa sana kwenye mitandao ya kijamii, tumezungumzia mambo mengi ikiwemo pia safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipofikia sasa ivi na jinsi gani kumpoteza mama ake kulimfanya apitie kipindi kigumu sana kwenye maisha yake. Ni matumaini yangu utafurahia mahojiano haya na pia kuna kitu utajifunza.

05-21
57:53

S03EP07 with Wakazi

Wakazi

03-12
01:54:45

S03EP06 with Gillsaint🧠

Gillsaint

03-05
55:41

S03EP05 with Mwaisa 🐒

Mwaisa

02-26
31:11

S03EP04 with Mr & Mrs Mrusi 💍

Episode hii nimeifanya special kwa ajili ya valentine kilichonifanya niwachague Mr & Mrs Mrusi ni kwa sababu wapenzi hawa twitter ndo iliwakutanisha kwa mara ya kwanza na baada ya hapo kufikia maamuzi ya kuoana, kwenye Episode hii tumezungumza mambo mengi kuhusu mahusiano na ndoa vile vile tumegusia maisha ya wawili hawa ndani ya ndoa. #PHONECALLBYFOTTY

02-15
48:19

S03EP03 with Jabir Saleh

Jabir Saleh

01-29
42:14

S03EP02 with Bajabir

Bajabir

01-22
37:32

S03EP01 with Madenge

Madenge

01-15
43:24

S02EP04 with Jalilu Zaid

Jalilu

08-07
28:01

S02EP03 with Chapo

Chapo

07-24
28:08

S02EP02 with Geoffrey Lea

Geoffrey Lea ndio amehusika kwenye Episode hii ya 2 msimu wa 2 ni mchambuzi na mtangazaji wa michezo kutokea Efm, Kwenye Episode hii tumeongea mambo mengi kuhusu mpira wa miguu lakini vile vile mpira wa kikapu sababu yeye ni mpenzi wa kikapu pia vilevile ukiachana na hayo tuliongea kwa jinsi gani Mama ake (M/Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) amekua na mchango mkubwa sana katika safari yake hii. Kama wewe ni kijana ambae unajihusisha na jambo lolote lile katika Episode hii utajifunza kutokukata tamaa na kufanikisha lengo ulilokua nalo. #PHONECALLBYFOTTY

07-17
27:03

S02EP01 with COCO

Coco

07-03
26:16

S01EP10 with Fred Kavishe

Fred Kavishe mmoja wa waanzilishi wa TOT BONANZA (Tanzania On Twitter) bonanza kubwa linalowakutanisha watumiaji wa twitter sehemu moja ili kuweza kujuana zaidi na kuenjoy, Kwenye Episode hii tumeongelea mambo mengi sana kuhusu Bonanza hili kuanzishwa kwake,Changamoto na mambo mengi sana. Vilevile tulipiga story na Fred juu ya safari yake ya Kupunguza uzito kutoka kilo 105 mpka kilo 65 ambayo ndo anamaintain sasa ivi. #PHONECALLBYFOTTY

06-05
26:29

S01EP09 with Shamira Mshangama

Shamira Mshangama ni Mkurugenzi mtendaji na Muanzilishi wa Tasisi ya (Mwanamke na Uongozi) ni tasisi isiyokua ya kiserikali (NGO), yenye kazi ya kuhamasisha wasichana wenye Umri kuanzia miaka 12 kushiriki nafasi mbali mbali za uamuzi na kugombea Uongozi. Kwenye Episode hii tumeongea mambo mengi sana kuhusu Wanawake na changamoto gani wanazipata kwenye jamii yao. Vile vile nilipata nafasi ya kupiga story na Shamira kuhusu maisha yake binafsi.

05-29
28:24

Recommend Channels