Discover
SBS Swahili - SBS Swahili
SBS Swahili - SBS Swahili
Author: SBS
Subscribed: 193Played: 11,418Subscribe
Share
© Copyright 2025, Special Broadcasting Services
Description
Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili
1493 Episodes
Reverse
Mipango inafanywa kupeleka wauguzi zaidi katika Wilaya ya Kaskazini kujibu mlipuko mbaya zaidi wa diphtheria nchini kwa zaidi ya miaka 30.Kesi 230 za maambukizo zimeripotiwa mwaka huu, kesi nyingi zikiwa katika Wilaya ya Kaskazini, lakini pia katika majimbo ya Magharibi Australia, Kusini Australia na Queensland.Nchini Uganda, zaidi ya watu 100 wamewekwa karantini, baada ya kushukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, wakati huu serikali ikiweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo, baada ya watu wawili kuthibitishwa kuambukizwa jijini Kampala.Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ni dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi kimataifa.WHO inasema mlipuko huo hauja fikia vigezo vya dharura ya janga, lakini nchi zinazo changia mipaka ya ardhi na DRC ziko katika hatari kubwa ya usambaaji zaidi.Kwa wakazi wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekuwa na mambo mengi ya kuhofia kutokana na uhasama ambao umekuwa ukiendelea kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji waasi.Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.
Je, unajua jinsi yakuomba msaada kwa Kiingereza bomba zako nyumbani zikipata tatizo?Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapaBonyeza hapo juu kwa mafunzo ya Kiingereza chepesi, kuhusu namna ya kuzungumza kuhusu bomba ambazo zina matatizo nyumbani kwako.
Waziri wa Afya Mark Butler ametetea utoaji wa kifurushi cha dola milioni 7 kutoka kwa serikali kusaidia kujibu mlipuko wa ugonjwa wa diphtheria ambayo ni maambukizi makubwa ya bakteria yanayoambukiza sana na huathiri njia zakupumua na inaweza sababisha vidonda kwenye mwili pia.Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Australia kimepanda hadi asilimia 4.5, huku kazi 19,000 zikiaondoka katika uchumi mnamo Aprili. Ofisi ya Takwimu ya Australia inasema ongezeko la ukosefu wa ajira imechangiwa na kupungua kwa ajira ya wanawake, kushuka kwa kwanza katika kitengo hicho tangu Agosti 2025.Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko wa Ebola ambao tayari umesababisha vifo vya watu 130 nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huenda ulianza miezi miwili iliyopita.Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi.
Fuel prices have spiked, and so have concerns and complaints about alleged price gouging. Are retailers cashing in on the crisis? - Bei za mafuta zimepanda, na wasiwasi pamoja na malalamiko kuhusu madai ya kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji nao pia ume ongezeka. Je, wauzaji wa rejareja wanafaidika kupitia mgogoro huu?
Kuto simamia mali vizuri, kunaweza weka mahusiano na familia nyingi katika hali mbaya.Anne Mureithi hutoa mafunzo kwa familia na jinsi yaku kuza mali zao. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Bi Anne alichangia mbinu ambazo familia zinaweza tumia kuimarisha familia na mali zao.Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.
Serikali ya Australia imeanzisha hatua kadhaa za kusaidia kupunguza shinikizo la usambazaji wa mafuta linalo endelea.Hatua hizo zinajumuisha kupunguzwa kwa muda kwa ushuru wa mafuta, na mamlaka zaidi kwa ACCC kupambana na kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji.Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi
Mbunge wa chama cha Liberal Andrew McLachlan anasema Upinzani wa Mseto haufai kutafuta mwongozo kutoka kwa chama cha One Nation kuhusu maendeleo ya sera zao, huku akiendelea kupinga pendekezo la Angus Taylor la kupunguza malipo ya ustawi wa jamii kwa watu ambao si raia.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema Jumatatu itafungua vituo vitatu vya matibabu, kwa ajili ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika jimbo la Ituri.
Mjadala unaendelea kuhusu mustakabali wa mfumo wa kodi wa Australia, baada yakutolewa kwa bajejeti ya Shirikisho wiki iliyopita.
Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC iliyoko mjini The Hague, Uholanzi imesema mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda Felicien Kabuga amefariki dunia.
Waziri wa Fedha Jim Chalmers ame ongeza mashambulizi ya chama cha Labor dhidi ya hotuba ya majibu ya bajeti ya Angus Taylor, akimshtumu kiongozi huyo wa Upinzani kwa kutoa pendekezo lenye madeni, upungufu wa kifedha, na utengano.
Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu.Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu.
Upunguzaji wa fedha katika Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu ndio chanzo kikubwa zaidi cha uokoaji wa fedha katika bajeti ya serikali shirikisho, jambo linalowaacha watu wengi katika jamii ya wenye ulemavu wakiwa na hasira na wasiwasi juu ya kile kinachokuja.
Serikali ya Ghana imetangaza kuwa itawarudisha raia wake 300-wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia ongezeko la visa vya wageni kushambuliwa.
Mmoja wa matajiri wakubwa barani Afrika Aliko Dangote, ameonesha nia yakuanzisha kiwanda chaku safisha mafuta nchini Kenya.
Utafiti mkubwa zaidi nchini Australia kuhusu mazingira ya kazi ya wahamiaji umefichua maelezo ya kutisha ya malipo duni yaliyoenea na ya kimfumo.
Mweka Hazina wa taifa, Jim Chalmers, ameelezea bajeti inayokuja kama ile yenye malengo makubwa zaidi ya serikali ya Labor kufikia sasa, ikiwa na kile anachokiita akiba na mageuzi makubwa kuliko kawaida.
Kirusi cha Influenza ni aina ya mafua yanayo ambukizwa kwa urahisi mkubwa na huzunguka mwaka mzima, lakini shughuli za mafua huongezeka wakati wa vuli, na maambukizi hufika kilele chake katika miezi ya majira ya baridi.
Waziri wa Makazi Clare O'Neil, anasema bajeti ya shirikisho itasaidia sana kushughulikia upungufu wa usambazaji wa makazi.























