Discover
Sepetuko

154 Episodes
Reverse
Matukio yanayoendelea ndani ya chama cha UDA ni dhihirisho tosha la umbali wa safari yetu kuwa na vyama vya kisiasa vyenye sera na msimamo. Vyetu ni vyama vinavyotumiwa tu kuwa daraja la kuingia mamlakani na baada ya uchaguzi, kudondoshwa kama kaa moto.
Bunge la Kitaifa linaanza kuwapiga msasa Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto, katika Baraza jipya alilotangaza. Hii ni fursa adimu kwa Bunge kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba na kuonesha kuwa ni taasisi huru na inayojisimamia bila kushurutishwa na Serikali tendaji. Hii ni fursa ya Bunge kusafisha jina lake ambalo limekuwa si lolote la kujivunia.
Chama cha ODM kimeendelea kutoa msimamo kinzani kuhusu hatua ya viongozi wake wakuu kujumuishwa serikalini, na kuibua kumbukumbu ya hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Wabunge wake waliotangaza msimamo wao wa kushirikiana na serikali baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Je, viongozi hawa wakuu wa chama hiki watachukuliwa hatua zozote. Kama sivyo, basi tusihadaiwe zaidi.
Maandamano yaliyofanywa na wanahabari nchini hayashinikizi lolote nje ya Katiba ya nchi. Yanashinikiza tu taaluma ya uanahabari kuheshimiwa na haki za wanahabari kulindwa kama ilivyo katika sheria za nchi. Wanahabari sio wahalifu, wao ni mwito wa kuitumikia nchi na wananchi wake.
Maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali yanamaanisha kuwa Rais William Ruto atastahili kuwasikiliza zaidi vijana wanaoandamana. Kusikiliza huku hakuwezekani katika mazingiraya kujipiga kifua na vitisho. Kusikiliza huku ni zaidi kupitia kwa matendo.
Harakati ambayo imekuwa ikiendelezwa dhidi ya serikali lazima ikuze taifa linalosikiliza. Linalosikiliza kwa lengo la kuelewa, na kukumbuka kuwa serikali ni raia na sio vinginevyo. Government by the people, for the people...
Maandamano dhidi ya serikali yameingiliwa na wahuni ambao nia yao ni kupora, kujeruhi na hata kuua na kuharibu. Jumatano wiki hii, wahuni pia wametatiza mkutano wa Azimio, wakisababisha purukushani na majeraha kwa wanahabari.
Ni wakati wahuni hawa na wafadhili wao wakabiliwe vilivyo.
Kukamatwa kwa mwanahabari mtajika Macharia Gaitho katika mazingira ya kudhalilisha na kuhujumu haki za mtu, siku moja tu baada ya mwanahabari wa Kameme kufyatuliwa risasi na polisi huko Nakuru alipokuwa akiangazia maandamano dhidi ya serikali kunaonesha kuchipuka tena kwa majaribio ya kudunisha uhuru wa vyombo vya habari unaolindwa Kikatiba.
Kamwe tusikubali hilo kufanyika, uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari ni mhimili muhimu mno wa demokrasia ya Kenya.
Tukio la kufyatuliwa risasi mwanahabari wa Kituo cha Kameme Nakuru Wanjeri wa Kariuki katika maandamano dhidi ya serikali ni mfano hai wa majaribio ya serikali kuwalenga wanahabari, kwa lengo la kuwanyamazisha wasitekeleze wajibu wao ambao unalindwa na Katiba ya Kenya.
Kamwe hatuko tayari kurudisha nyuma hatua kubwa zilizopigwa katika kukuza demokrasia na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.
Tukio la kupatikana miili zaidi ya tisa eneo la Kware, Embakasi ni dhihirisho tosha la nchi ambayo taasisi zake za kiusalama hazifanyi kazi, zimefeli pakubwa. Iweje watu wauliwe na miili yao kutupwa bila NIS, DCI au Idara ya Polisi kuwa na ufahamu ya tukio hilo la kihalifu? Tunataka uwajibishwaji wa ofisi husika.
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amewaandikia Mawaziri wote kuwataka kupunguza idadi ya washauri kutoka wawili hadi mmoja kwa kila Waziri ili kupunguza matumizi ya pesa za serikali. Hatua hii imeibua swali la hivi hawa washauri wamekuwa wakifanya kazi gani ikiwa kwa kipindi cha miaka miwili serikali hii imekuwa ikifanya baadhi ya maamuzi mabovu mno, kiasi cha kugeuka na kuwa shubiri kiasi hiki? Je, washauri hawa wamefeli katika majukumu yao au ushauri wao umekuwa ukipuuzwa na viongozi wanaoshauriwa?
Miaka sitini tangu kupata uhuru uongozi wa nchi ya Kenya umekuwa ukiendeshwa na wanasiasa wabinafsi wasiomjali yeyote ila maslahi yao tu.
Hali inaonekana inabadilika na sasa wananchi wataanza kujiamulia wanavyotaka kuongozwa. Hilo lifanyikapo, basi ole wao hawa wanasiasa. Interesting times ahead!
Maafisa wa Kliniki wametamatisha mgomo wao ambao umedumu siku 99 baada ya mapatano kati yao na Baraza la Magavana COG. Hii ni nafuu kubwa kwa Wakenya ambao hutegemea huduma katika hospitali za umma, japo inatoa changamoto kwa serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa migomo hii ya mara kwa mara katika sekta ya afya.
Sepetuko leo inahongera serikali kwa hatua yake ya kubadili mwenendo na kuanza kuwasikiliza raia.
Ni katika kuwasikiliza raia ndipo serikali itaweza kuafiki mengi, na sio katika kuwapuuza wananchi ambao ndio wenye serikali.
Viwango vya unyenyekevu miongoni mwa wanasiasa wetu, ambavyo vinashuhudiwa baada ya maandamano na harakati za vijana wa kizazi cha Gen Zs na wengine ni mfano hai wa uwezo wa watu. Yaani hadi wanasiasa wetu wenyewe wanakataa nyongeza ya mishahara waliyokuwa wameongezewa na Tume ya Utathmini wa Mishahara na Marupurupu SRC! Huu unafaa kusalia kuwa mkondo. Wanasiasa kujua kuwa kuipuuza sauti ya mwananchi ni kujiweka taabani.
Maandamano yanayoendelezwa nchini dhidi ya serikali yanalindwa na Katiba ya Kenya, bora tu yafanywe kwa amani. Inasikitisha kuwaona wahuni wakihitilafiana na maandamano haya, kuwapora Wakenya mali yao waliyoitafuta kwa jasho lao. Wacha watuhumiwa hawa wasakwe na kukabiliwa na mkono wa sheria kutokana na shughuli zao za kihalifu. Hawa sio sehemu ya waandamanaji na kamwe hawafai kuchukuliwa hivyo.
Visa vinavyoendelezwa na serikali vya kuwateka nyara vijana na wanasiasa wanaohusishwa na maandamano dhidi ya serikali yanatia shubiri uwezekano wa kufumbua fumbo hili. Zaidi ni uhuni ambao ni kinyume kabisa na sheria za nchi. Amani haipatikana kwa kiganja kilichofumbatwa.
Sehemu kubwa ya matatizo yanayokumba serikali hii ni Wakenya kukosa imani kwake kutokana na kuwapo Rais asiyependa ukweli. Rais ambaye hadi leo amekwama katika uongo wa kuwatetea maafisa wa usalama waliohusika katika ukatili dhidi ya waandamanaji. Rais anayesema hili, kisha naye anafanya jingine. Ni hadi Rais Ruto amaanishe ayasemayo, afanye anayosema na ajifundishe kusema ukweli ndipo hali hii ya sasa itaimarika.
Vijana wa Gen Zs na vijana wengine ambao wamekuwa wakiendeleza maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 wametukumbusha uwezo tulio nao kama wananchi wapigakura. Uwezo wa kupiga kura kuwachagua viongozi wetu, lakini zaidi kuwawajibisha wanapokuwa ofisini. Harakati hii haifai kukoma. Huu unafaa kuwa mwanzo tu wa kutetea Katiba yetu na kudai uongozi bora ambao tunastahili.
Hatua ya serikali kuwatuma wanajeshi kusaidia polisi kuwakabili waandamanaji ni ukiukaji mkubwa wa sheria za nchi. Inasikitisha kuwa Bunge la Kitaifa limetumiwa kutia muhuri uhayani huu! So unfortunate!