Kama Mazoea kwa Ngoswe, vivyo hivyo Brooke Shields kwa Andre Agassi.--Utofauti uliopo ni kuwa, karatasi za sensa za maisha ya Andre, ziliokolewa na huba la Steffi Graf.Kama ile ya Romeo na Julieth, hii nayo ni simulizi ya wapendanao--Tafadhali Isikilize.
Historia nyuma ya uanzishwaji wa chuo/taasisi ya teknolojia ya Armour, yaani "Armour Institute of Technology" (Kwa sasa: Illinois Institute of Technology), haianzii katika ukatwaji wa utepe kwenye ile siku ya ufunguzi wa milango ya chuo hicho ya September, 1893. Historia yake inarudi nyuma kidogo, mpaka kwenye ile asubuhi ya jumapili moja, ndani ya ibada ya kanisa la 'Plymouth Church'.Hii ni simulizi fupi ya namna ambavyo maono yaliyokuwa yamejificha ndani ya moyo wa kijana mmoja, yalivyozaa hiyo taasisi ya elimu--Tafadhali isikilize.
Historia inamtaja Sir Edmund Hillary kama mtu wa kwanza kufanikiwa kuukwea Mlima Everest hata katika kilele chake. Hii ni simulizi nzuri, nyuma ya hiyo safari yake ya matumaini.
Kabla ya kuanza kuisifu ile ming'ao ya zile medali zinazoning'inia shingoni mwa wanariadha nguli kama Usain Bolt, Alphonce Simbu, Eliud Kipchoge nakadhalika--Kuna kitu cha kukisifu kwanza, hususani kwenye ulimwengu wa ukimbiaji--Ni miguu ya yule msichana, iliyokimbia riadha ya ndani ya uwanja na ndani ya kilindi cha moyo wa binti mdogo aliyekuwa na ndoto kubwa.Tafadhali sikiliza simulizi hii fupi ya mwanariadha, Elizabeth Robinson Shwartz.
Wakati vita kuu ya pili ya dunia ikiendelea, kuna baadhi ya watu walijitoa sana kupigana kwaajili ya maisha ya wengine. Inasikitisha kuona hawatajwi katika vitabu vya kihistoria ilihali walikuwa na mchango mkubwa katika maisha ya wengi.Tafadhali sikiliza kwa umakini episode hii, ili kuthamini mchango wa baadhi ya mashujaa hao wasioimbwa ipasavyo.