DiscoverWimbi la Siasa
Wimbi la Siasa
Claim Ownership

Wimbi la Siasa

Author: RFI Kiswahili

Subscribed: 12Played: 802
Share

Description

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

201 Episodes
Reverse
Watanzania wanapiga kura kuwachagua wabunge, madiwani na rais, katika uchaguzi ambao rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuibuka mshindi, baada ya mpinzani wake mkuu Tundu Lissu, kuzuiwa jela na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, anakutana na wanasiasa wa upinzani jijini Nairobi, kuanzia Oktoba 14,  wiki mbili baada ya kuhukumiwa kifo na Mahakama ya kijeshi. Wanasiasa hao wanazungumza nini ? Tunachambua.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa waasi wa AFC/M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi,  katika maeneo wanayodhibiti, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa Washington uliokubaliwa kati ya DRC na Rwanda kuhusu namna ya kupata mwafaka wa kudumu. Hatua hii inamaanisha nini ? Tunachambua. 
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uganda, uliopangwa kufanyika Januari 12, 2026, zilianza Septemba 29. Kuna wagombea wanane wa urais, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 39. Mpinzani wake mkuu ni Robert Kyagulanyi  maarufu kama Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 43. Nini kinachotarajiwa kwenye kampeni hizi ?
Vital Kamerhe, Septemba 22, alijiuzulu kama Spika wa Bunge la taifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kuundwa kwa Tume ya kumchunguza dhidi ya madai ya matumizi mabaya ya madaraka, kuwahangaisha wabunge na kuwalazimisha kupitisha miswada haraka haraka.Nini hatima ya kisiasa ya Kamerhe baada ya kujiuzulu ? Ataendeleza ushirikiano wake wa karibu na rais Felix Tshisekedi ?
Nchini Sudan Kusini, serikali ya rais Salva Kiir, imetangaza kumfungulia mashtaka ya uhaini na uhalifu wa kivita, kiongozi wa upinzani Riek Machar, ambaye ameondolewa kwenye nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais, kufuatia shambulio la wapiganaji wa White Army kwenye kambi ya jeshi katika  jimbo la Upper Nile mwezi Machi mwaka 2025. Nini hatima ya Machar na Sudan Kusini ?
Mji wa Uvira, jimboni Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa zaidi ya wiki moja, ikiwemo Septemba 08, umeshuhudia maandamano yaliyopangwa na mashirika ya kiraia na wapiganaji wa Wazalendo, kupinga kupinga kuteuliwa kwa Jenerali Olivier Gasita, kuwa Naibu Kamanda wa Kikosi cha jeshi la FARDC, katika eneo hilo kwa madai ya kuwa na ushirikiano na waasi wa AFC/M23 kwa sababu ya kabila lake la Banyamulenge.
Tanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu kuanzia Agosti 28, kuelekea kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025. Rais Samia Suluhu Hassan, kutoka chama tawala CCM, anawania uongozi wa nchi hiyo. Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea  kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.
Rais wa Marekani Donald Trump, amechukua hatua ya kuongoza harakati za kumaliza vita vya miaka mitatu vya Urusi nchini Ukraine. Trump amekutana na rais Vladimir Putin na Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine pamoja na viongozi wengine wa nchi za Ulaya  Agosti 18, baada ya awali kukutana na rais Putin Agosti 15 jimboni Alaska. Je, Trump atafanikiwa  kumaliza vita hivyo ?
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23/AFC, Julai 19, walitia saini rasimu ya makubaliano jijini Doha nchini Qatar ya namna ya kusitisha vita Mashariki mwa DRC na kupata amani ya kudumu. Ni mambo yepi yaliyokubaliwa na changamoto zipi zinazokabili pande hizi mbili kwenye utekelezwaji ? Tunajadili.
Kiongozi wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80, ameteuliwa na chama chake cha NRM, kugombea tena urais wakati wa uchaguzi mkuu uliopagwa kufanyika mapema mwaka 2026, baada ya kuwa madarakani miaka 40. Hii inamaanisha nini katika siasa za Uganda ?
Vijana nchini Kenya maarufu kama Gen Z, wameendelea kuandamana dhidi ya serikali ya rais William Ruto. Maandamano haya yameishia kwenye maafa na majeruhi tangu mwezi Juni mwaka 2024. Tunaungana na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha NIBS kilichopo Ruiru, kusikia kutoka kwao. Kwanini wanaandamana ?
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, walitia saini mkataba wa amani, chini ya uangalizi wa Marekani, Juni Juni 27 2025, jijini Washington DC, unaolenga kurejesha amani ya kudumu Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kuyaondoa makundi yenye silaha. Mkataba huu umepokelewa vipi nchini DRC ?
Israel na Iran zimekubali pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump, kuacha kushambuliana baada ya vita vya siku 12 vilivyosababisha vifo zaidi ya 600 nchini Iran na zaidi ya 20 nchini Israeli. Israeli ilianza mashambulio hayo, kwa kulenga vituo vya  nyuklia vya Iran  kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha za maangamizi. Je, usitishwaji huu wa vita utadumu ?
Serikali ya Kenya mwezi Januari 2025, ilisaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na nchi ya Falme za Kiarabu kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Mswada huo umezua pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharakati, watunga será na wapinzani wa serikali na wanataka wabunge kuufanyia marekebisho. Je, kuna siasa gani kwenye mikataba ya Kimataifa inayotiwa saini kati ya serikali ya Kenya na nchi za kigeni ? Edgar Odari Mkurugenzi Mkuu wa, Econews Africa, na Torosterdt Alenga mchambuzi wa siasa za Kimataifa, wanathathmini.
Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza raia wa nchi 12 hasa kutoka Afrika kutozuru nchi hiyo. Agizo hilo lilianza kutekelezwa Juni 9, 2025. Trump anasema amechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama. Wakati hayo yakijiri, maandamano yamekuwa yakishuhudiwa katika mji wa Los Angeles, kupinga sera ya Trump ya kuwasaka na kuwafukuza nchini humo, wageni wanaoishi bila vibali. Tunachambua kwa kina.
Uongozi wa kijeshi nchini Sudan mwishoni mwa mwezi Mei, ulimteua mwanasiasa  na mwanadiplomasia mkongwe Kamil Idris, kuwa Waziri Mkuu mpya wakati huu vita vikiendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. Tangu kuanza kwa vita Aprili 2023, watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha, huku wengine Milioni 15 wakikimbia makaazi yao, wakiwemo zaidi ya Milioni nne ambao wamekimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Nini hatima ya Sudan ?
Maseneta nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemwondolea kinga ya kutoshtakiwa  rais wa zamani Joseph Kabila , ambaye ripoti zinasema alirejea Goma usiku wa Mei 25.Kiongozi huyo wa zamani, ameishtumu serikali ya rais Felix Tshisekedi na kuuita ya  Kidikteta. Hata hivyo, serikali ambayo inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kushirikiana na waasi wa M23.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, akiwemo Martha Karua na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, walifukuzwa nchini Tanzania, Mei 19, walikokuwa wamekwenda kama mashuhuda wa kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa nchi yake haitaruhusu wanaharakati kutoka nje, kuvunja amani ya nchi yake. Tunachambua kilichotokea nchini Tanzania.
Mswada tata, utakaoruhusu raia wa kawaida kushatakiwa kwenye Mahakama za kijeshi, umewasilishwa bungeni nchini Uganda, Mei 13, 2025. Upinzani unasema, lengo la mswada huo ni kuwalenga wanaopinga kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2026. Kwanini serikali ya Uganda inataka raia wa kawaida washtakiwe kwenye Mahakama za kijeshi ?
loading
Comments