06 NOVEMBA 2025
Update: 2025-11-06
Description
Hii leo katika Habari za UN tunakuleta Muhtasari wa Habari ukimulika kuanzishwa kwa Taasisi ya kusaidia uhifadhi wa misitu ya kitropiki, TFFF huko Brazil ambako kutaanza mkutano wa COP30 tarehe 11 mwezi huu wa Novemba. Halikadhalika kuna kauli ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu kuanzishwa kwa taasisi hiyo. Muhtasari unamulika pia kuporomoka kwa kilimo cha afyuni nchini Afghanistan.
Mada kwa kina inamulika jinsi shirika la kiraia la Global Youth Forum linavyotumia kandanda au mpira wa miguu kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
Katika Jifunze lugha ya Kiswahili, Mlumbi Joramu Nkumbi anafafanua maana ya maneno, Jamala na Bulbul.
Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.
Comments
In Channel

















