DiscoverENKYFRANK
ENKYFRANK
Claim Ownership

ENKYFRANK

Author: Frank Pande

Subscribed: 1Played: 3
Share

Description

A 24/7Writer
Podcaster
SocialMediaExpert
ContentCreator
13 Episodes
Reverse
Miaka 35 Ya Muziki Wa Dr. Dre, Familia Na Utajiri Wake by Frank Pande
Utajiri wa Wiz Khalifa unatajwa kuwa dola milioni 45 sawa na shilingi bilioni 1.5. Jina la Wiz Khalifa lipo kwenye orodha ya wanamuziki 50 wa Hip Hop wenye mkwanja mrefu.
Harmonize Amewakosea Mashabiki, Hakuna Kama Uno by Frank Pande
Kisuswe - Shaku

Kisuswe - Shaku

2020-01-3002:34

Kisuswe - Shaku by Frank Pande
Diamond amekuwa msanii namba moja kwenye kila nchi Afrika Mashariki kwa muda mrefu bila kupoa, sio rahisi kwa msanii ambaye nyuma yake kuna wasanii wengine zaidi ya watano ambao wote wapo chini ya LABEL yake na Brand zao ni kubwa zinazohitaji gharama kuziendesha. Diamond amekuwa msanii ambaye amekutana na changamoto nyingi kwenye muziki wake ikiwemo kufungiwa nyimbo zake na baraza la sanaa pamoja na baadhi ya vituo vya radio na TV kitu ambacho hakijawahi kumfanya asite kuendelea kufanya kazi zake katika mtindo ambao mashabiki wake wanataka kumsikia na kumuona.
Mashabiki wamekuwa na mitazamo tofauti baada ya hiki kinachoendelea wengine wakifananisha tukio hili na tofauti kati ya Uongozi wa WCB na Harmonize, Ikiwa hakuna hata mmoja kati yao ambaye anaonyesha ishara ya kutokuwepo na tofauti basi mashabiki wa WCB na Harmonize msijigawe. Kinachoendelea hapa ni biashara, Harmonize amemaliza kukifanya alichoweza kukifanya akiwa WASAFI, kama ni pesa ameingiza ya kutosha na hata viongozi wa WCB wameridhishwa na alichokifanya chini ya uongozi wao. Ifahamike kwamba ni kitu cha kawaida kwa mwanamuziki kuondoka kwenye Label aliyomaliza nayo mkataba hata kama Label hiyo inamilikwa na baba yake mzazi. Kila mtu ana mipango na malengo aliyojiwekea kwa ajili ya kuendeleza maisha ili kujikwamua kiuchumi.
Maajabu 12 Ya Harmonize Chini Ya WCB Wasafi by Frank Pande
#Whozu ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wa Karne hii wenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa vijana wa umri wake. We wish him all the best, Tunapenda kuona anakua siku hadi siku na hatimae kuingia soko la kimataifa na kuendelea ku-Inspire vijana wenzake wanaomuangalia kama Role Model kwa sasa.
Damini Ogulu amezaliwa Julai 2.1991, ni mwanamuziki wa Nigeria mwenye uwezo wa kuimba na kuandika nyimbo zake mwenyewe. Umaarufu ulimsogelea mwka 2012 baada ya kuachia wimbo ulioitwa ‘Like to Party’ kutokea kwenye Albamu yake iliyopewa jina L.I.F.E ya mwaka 2013 na kuanzia hapo Burna Boy ni miongoni mwa wanamuziki muhimu Afrika. Albamu yake ya kwanza yenye nyimbo kama ‘Yawa Dey, Run My Race, Always Love You, Tonight na Lead single ‘Like To Party iliachiwa Agosti 12,2013 iliuza kopi 40,000 siku yake ya kwanza sokoni. Albamu hiyo ambayo iliandaliwa na producer Leriq, ilikuwa na kolabo za wasanii wengine wakubwa Nigeria akiwemo 2baba Idibia, M.I Abaga, Timaya, Olamide na Wizkid. Mtandao wa Nigeria Entertainment Today uliipa Albamu hiyo nafasi ya 10 kwenye Albamu 12 zilizofanya vizuri Nigeria mwaka 2013. Aina ya muziki uliotumika kwenye Life ulikuwa ni aina ya Muziki uliofanyika miaka ya nyuma na wakongwe kama Fela Kuti, King Sunny Ade na Bob Marley. Albamu hiyo ilipata Positive Feedback kutokea kwa wakosoaji wa muziki kutokana na uandaaji wake ambao ulionekana kuwa kivutio kwa mashabiki na wadau wa muziki kwa ujumla. Burna Boy alitajwa kuwania tuzo ya Albamu bora ya mwaka 2013 Nigeria kupitia L.I.F.E Albamu ambayo ilifanikiwa kushika nafasi ya 7 kwenye chati ya Billboard Reggae. Wakati wote huo Burna Boy alikuwa ni msanii ambaye kazi zake zilikuwa zikisimamiwa na Aristokrat Records ambayo aliachana nayo mwaka 2014 na kuanzisha Label yake iliyoitwa Spaceship Entertainment. Albamu yake ya pili On A Spaceship iliachiwa 2015, ilifuatiwa na Redemtion EP yenye nyimbo 7 aliyoiachia September 2016, Mwaka 2017, Burna Boy alisaini mkataba wa kurekodi na Atlantic Records ya Marekani ambayo inafanya kazi na wanamuziki kama Future, Young Thug, Migos na wakali wengine wengi. January 2018, Burna Boy aliiachia Albamu yake ya 3 Outside, ambayo aliioifananisha na Mixtape. Outside ni Albamu ambayo muziki wake una ladha mchanganyiko za Afrobeats, Dancehall, na Reggae. Albamu hiyo ilipewa sifa nyingi na wachambuzi wa masuala ya muziki, na mitandao mingi Nigeria ziliipa heshima kama Albamu bora ya Kinigeria kwa mwaka 2018. Outside ilishinda tuzo ya Albam bora ya mwaka kwenye Nigeria Entertainment Awards huku moja kati ya ngoma zake ‘Ye’ ikimaliza kama ngoma kubwa ya mwaka 2018 Nigeria. June 2018, Burna Boy alisaini mkataba wa kusambaza kazi zake na Universal Music, Mwezi oktoba 2018 alitangazwa kama mwanamuziki mpya wa Afropop anaesikilizwa huku YouTube pia wakimtaja kama Msanii ambaye nyota yake inan’gaa kwenye mtandao huo ambao kwa miaka 14 sasa umekuwa sehemu ya maisha ya wanamuziki wote duniani ambao wanautegemea kwa kusambaza video za kazi zao. Januari, 2019 Burna Boy na Mr Eazi walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotajwa kufanya Perfomance kwenye Coachella Valley Music and Arts Festival. Mwezi machi 2019 Burna Boy aliiachia Steel & Copper, EP yenye nyimbo 4 ambayo alishirikiana na kundi la DJDS la Marekani. Taarifa za ujio wa Albamu yake ya 4 African Giant zilianza kusambaa tangu mwezi April mwaka huu na hatimaye muda wa kusubiri umeisha. African Giant imeingia sokoni Julai 26 ikiwa na ngoma 19 zikiwemo Gbona, Anybody, Dangote na On The Low ambazo zimeendelea kufanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Damian Marley, Jorja Smith, Future na YG ni miongoni mwa mastaa walioibariki Albamu hiyo kwa kushirikiana na Burna Boy kwenye baadhi ya ngoma ambazo huenda zikafanya vizuri kama zilizotangulia. Katika kipindi cha miaka 8 kwenye muziki, Burna Boy amefanikiwa kuachia single 25, Albamu 4, Mixtape 2 EP 2 na video 11 za nyimbo zake ambazo zimewahi kufanya vizuri. Burna Boy ni mshindi wa Tuzo 9 kati ya 15 ambazo amewahi kuwania ikiwemo Best International Act ya BET ambayo alishinda June 24,2019.
Haumpati kwenye headlines za udaku, haumkuti kwenye trend za kiki wala interviews zisizoeleweka, Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Timu yake imekua makini sana kumuweka mbali na umaarufu wa skendo.
Tamasha la Castle Lite Unlocks limefanyika Dar Es Salaam jumamosi ya Wikiendi iliyopita yaani Julai 20 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama. Mkali wa Rap ya Wasichana hapa namzungumzia Rosa Ree, aliungana na wasanii kama Wakazi, Ay na Mwana FA kuamsha wahudhuriaji wa tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama. Yule Boi, Ghaddafi, Country Wiz Aka FatherOfNewGeneration alikuwepo stejini pia huku akipata support ya kutosha kutokea kwa mashabiki mpaka washikaji akiwemo Prodyuza S2Kizzy ambae amekua akifanya nae kazi kwa ukaribu. Country Boy ameonyesha energy ya hali ya juu kwa kuhudumia stage tatu za nguvu ndani ya Wikiendi moja. Ijumaa iliyopita Country Boy alikuwamiongoni mwa wasanii waliofanya makamuzi kwenye stage ya Wasafi Festival msimu wa Pili ulioanzia Muleba mkoani Kagera. Baada ya kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa Kagera na maeneo yake ya jirani tayari akili ya Country Boy ilikuwa ikiwaza Safari ya Dar Es Salaam kwa ajili ya Castle Lite Unlocks. Wakati Jumamosi hapakuwa na ratiba ya Wasafi Festival, Ndio Country Wiz aliutumia kufanya yake kwenye Show ya Dar Es Salaam na jumapili ya Julai 21 Country Boy alikua Unyamwezini Tabora kukikamua kwenye Stage ya Wasafi Festival iliyofanyika mjini humo na kukamilika kwa asilimia nyingi. Country Boy amethibitisha kama nguvu ya muziki wake sio ya kitoto, Kitendo cha kuhudumia majukwaa matatu ya matamasha mawili tofauti ni heshima kwa muziki wake na ni uthibitisho kama Yule Boi anafanya kazi kubwa kuitangaza Trap ya Bongo.
Bila shaka ukipewa Pen na karatasi ili kuandika majina matano yanayofanya vizuri kwa beat kali mjini, Huwezi kusahau jina la S2Kizzy(Zombie) ambaye ameendelea kuwa mwiba wa Trap kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. S2Kizzy ameyafanya mengi kwa muda mfupi ambao amekuwepo, Haimaniishi wengine waliopita hawakufanya kazi nzuri bali S2Kizzy amechangia kuubadilisha mchezo wa Rap ambao ulikua haueleweki kipindi cha nyuma na kuwa kivutio zaidi kwa vijana wa umri wake. Ngoma kama ‘Wanaona Haya’ ya Country Boy, Pochi nene ya Rayvanny na 'Swagire' ya Weusi ni ushahidi unaotosha kuthibitisha kama tulihitaji uwezo wa S2Kizzy ili kuifanya Rap yetu iwe level tunayiona kwa sasa. Mbali na mchango wake kwenye Rap, utakubali kama Producer huyu ni zawadi yetu mashabiki wa Bongofleva kama umepata nafasi ya kusikiliza Ona ya Luludiva aliyomshirikisha Rich Mavoko. Ukiachana na ukubwa wa kolabo hiyo Utaweza kuona ni jinsi gani S2Kizzy aliwekeza muda wake kwa umakini akaikamilisha ngoma hiyo ambayo ilifanya vizuri ilipotoka na bado inaendelea kupata mashavu kwenye TV na Radio Station mbalimbali nchini. S2Kizy ameweza kucheza na hisia za mashabiki wengi wa Bongofleva sio kwa kutengeneza beats tu, bali hata uwezo wake wa kucheza na mizuka ya wanamuziki hata kujua jinsi ya kwenda nao sawa bila kuwakera mashabiki, Kauli hii naielekeza moja kwa moja kwa Giggy Money ambae tulianza kumfahamu kupitia Video za Bongofleva akawa star wa Instagram na hatimaye Giggy akawa msanii wa Bongofleva. Safari ya muziki wa Giggy inaweza kuwa miongoni mwa stori zinazoshawishi kwenye Industry, Kama Bongo tungekua na chati ya muziki inayoeleweka basi Giggy angepata wimbo wake wa kwanza kuwa namba moja Bongo baada ya kuiachia Nampa Papa ambayo ilitengenezwa na Producer Kimambo. Alichokifanya Giggy kwenye ‘Nampa Papa’ kinabaki kuwa historia kwake kwani uwezo aliounyesha kwenye ngoma hiyo ni mkubwa ukilinganisha na uzoefu aliokua nao kwenye muziki wakati huo. S2kizzy aliweza kuusoma mchezo wa Giggy na kufanikiwa kumshawishi Giggy kubadili gia angani, Collabo ya Giggy Money, Whozu na Sanja ‘Kiki Ni Gigi’ na ‘Good Time Drip’ ya Rj TheDJ zinatosha kutueleza kama wanapokuatana Giggy na S2kizzy huwa kinanuka mbaya. Giggy amekua mzuri zaidi kwenye Rap ukilinganisha na staili ya uimbaji aliyoanza nayo, Mashabiki wamemuelewa na wamekubali mabadiliko yake. Big shoutout kwa S2Kizzy. Kwa masikio yako unaweza kuzihesabu ngoma ambazo zimefanywa na S2kizzy halafu utagundua asilimia kubwa ni nyimbo zilizofanya vizuri kwenye chati za Radio mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Kolabo nyingine iliyotengenezwa na S2kizzy na kuonekana miongoni mwa ngoma kali ni ‘Far Away’ Diamond Platnumz inayopatikana kwenye Albamu yake ‘A Boy From Tandale’. Kwenye ‘Far Away’ S2kizzy kwa ushirikiano na Laizer w amewakutanishana Diamond pamoja na Vanessa Mdee kwenye beat moja na kuikamilisha ngoma hiyo ambayo kama itakuja kuachiwa itakuwa miongoni mwa ngoma kali zawakati huo. S2kizzy anaingia kwenye historia ya muziki wa Tanzania kwa kile ambacho amekifanya katika umri wake mdogo. Asilimia kubwa ya nyimbo alizofanya kama Producer zimesikilizwa mara nyingi na kulifanya jina la S2kizzy kusikika mara nyingi zaidi. Tunathubutu kusema S2kizzy ni miongoni mwa mashujaa na watetezi wa Bongofleva, Ni fahari kuwa na mtu kama yeye kwa wakati huu. Shoutout kwa King Luffa, Mr Ttouch,Kimambo, Ringtone, BreezyBeats na machalii wote waliokuja kipindi hiki, ubunifu wao ni muhimu zaidi. Washikaji wapo wanafanya kazi kubwa ili kutuburudisha sisi ambao mwisho wa siku tunaipata burudani hiyo bila gharama yeyote. Ipo haja ya kuwapa nguvu na kuwatahmini zaidi Maproducer wetu ili wazidi kuisogeza game yetu mbali na sisi muziki wetu ufike ile hatua tunauita wa Kimataifa.
KirahisiRahisi

KirahisiRahisi

2019-06-1603:08

KirahisiRahisi by Frank Pande
Comments 
loading
Download from Google Play
Download from App Store