DiscoverLearning by Ear – Elimu ya Jamii
Learning by Ear – Elimu ya Jamii
Claim Ownership

Learning by Ear – Elimu ya Jamii

Author: DW.COM | Deutsche Welle

Subscribed: 1Played: 25
Share

Description

Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.
41 Episodes
Reverse
Huku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.
Kila binaadamu hapa duniani ana haki ya uhuru na usawa - kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binaadamu. Lakini katika mataifa mengi barani Afrika, utakuta haki hizi zinaendelea kukanyagwa na kukiukwa.
Katika kipindi hiki, tutageuka na kuangazia sekta ya muziki na kupata nafasi ya kumfahamu Chimere Emejuobi, mwimbaji kutoka Lagos. Muziki ni muhimu sana katika jamii nchini Nigeria.
Hatutazungumzia juu ya taaluma fulani, lakini ni juu ya wale wote ambao hawana ajira. Idadi ya wasio na ajira hususan miongoni mwa vijana imeongezeka sana barani Afrika. Kila kijana mmoja kati ya watano hana ajira.
Katika mji mkuu wa Kenya, tunakutana na watu wanaofanya shughuli zao ambazo ziko nje ya sekta rasmi ya uchumi. Wanashughulika kinyume na sheria bila ya kuwa na elimu stahiki, mfano biashara ya kiwango cha rejareja.
Tutaiangazia sekta ya elimu huko Lagos Nigeria. Kwa jumla waalimu hulipwa mshahara mdogo. Lakini kwa baadhi yao, la muhimu ni hamasa ya kufundisha na hamu ya kuwapatia ufahamu wanafunzi wao.
Katika kipindi hiki tutapata nafasi ya kumfahamu kijana mmoja nchini Uganda ambaye ni meneja wa hoteli. Je kuna ugumu gani wa kufanya kazi ya umeneja wa hoteli katika nchi zinazoendelea kama Uganda?
Mtandao wa Intaneti ni lango kuu la kujiunga na jamii duniani. Hata hivyo bado watu wengi hawana uwezo wa kuitumia. Wafanyakazi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanajaribu kulibadilisha suala hili.
Kuna taaluma ambazo zinachukuliwa kuwa ni za wanaume tu. Ni wanawake wangapi wanaoweza kurekebisha magari au pikipiki? Estelle Christian Ouedraogo, kutoka Burkina Faso, ni miongoni mwao. Tujiunge naye!
Katika mfulululizo huu, tutakutambulisha kwa vijana wa kiafrika wenye taaluma mbalimbali, na kukupatia undani wa shughuli zao. Kwanza tutapata nafasi ya kumfahamu Judith ambaye ni nesi katika hospitali huko nchini Kenya.
“Wanaopata, wanaoweka. Anayepata kitu fulani njiani anaruhusiwa kukimiliki” Je, ni rahisi namna hiyo kila mara? Sikiliza hadithi ya kobe na tumbiri mjanja aliyelazimika kupata adhabu kuokoa mkia wake!
Hadithi yetu inatokea zamani za kale, wakati tausi alipokuwa angali mweupe. Jifunze jinsi alivyopata rangi zake nyingi na wakati huo huo kuiharibu sauti yake
Siku moja bundi mzee na nyenje kijana wanakuwa majirani. Mwanzoni wanafurahia kuishi kwa pamoja, lakini kadri muda unavyopita bundi anakasirika na nyenje anavunjika moyo. Watafanya nini?
Katika hadithi hii, marafiki zetu wanyama wenye njaa wanalazimika kutafuta njia ya kuchuma matunda mtini. Inaonekana kuwa kazi rahisi lakini mti wa maajabu wa marula unawafunza somo zuri
Mwanamke kizee akamwambia Amadou. “Usijiingize katika hali usizoweza kukabiliana nazo! Fuata maagizo yangu.” Lakini wakati mwingine inahitaji uhodari mkubwa mtu kukubali udhaifu wake, kama Amadou atakavyogundua
Kassi na Kaloo – marafiki wasioweza kutenganishwa! Angalau hali ilikuwa hivyo kabla farasi hao wawili wa kupendeza kupandwa na wafalme wawili mahasimu. Watafanya nini wakati vita vitakapozuka kati ya falme zinazopigana?
Je unaamini hirizi za bahati na mawe ya mazingaombwe? Sawa, zuia wazo hilo na tumruhusu ngiri atueleze hadithi yake kuhusu kilichomuokoa, na vipi
Fuata nyayo za Lipua! Njiwa jasiri ana kibarua cha umuhimu mkubwa. Je Lipua atamshinda mfalme mlafi na muovu Karamba na kuwaokoa ndege wenzake wasife kutokana na njaa?
Zamani paliondokea simba na fisi mwenye njaa. Kilichoanza kama uhusiano wa ajabu lakini wa furaha, kinamalizika huku fisi akiwa amejeruhiwa maisha yake yote na tai akipoteza manyoya yake kadhaa
Katika mfululizo mwingine wa kusisimua, tunautembelea ulimwengu wa mjusi kafiri Sindakh na chura aitwaye Mbott – hadithi kuhusu urafiki, uaminifu na usaliti
loading
Comments 
loading
Download from Google Play
Download from App Store