Zinga

<p>Kipindi cha asubuhi kwenye Radio Taifa, kuanzia Saa Kumi na Moja hadi Saa Nne.</p>

Serikali imejitolea kuwalinda wakenya dhidi ya majanga asema Mwanaisha Chidzuga

Naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga amesema serikali ya Rais William Ruto imejitolea kuhakikisha wakenya wanalindwa kutokana na majanga hasa mafuriko. Akiongea na Radio Taifa, Chidzunga amesema serikali imeweka mikakati mbali mbali kando na kuwahamisha wakenya na kuwapa makao wakenya walioathirika na mafuriko. Aidha amewasihi wakenya na mashirika mbali mbali kuungana ili kusaidia wakenya zaidi.

05-08
44:56

Zinga: Umuhimu wa Chanjo katika afya ya mwanadamu

Chanjo zimesaidia kuokoa maisha mamilioni ya watu duniani kote katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, zimekuwa ni hakikisho kwa makuzi salama ya watoto na afya bora kwa watu wazima.Hata hivyo, wataalamu wamebaini hali ya ongezeko la kukataa kutumia chanjo katika baadhi ya maeneo duniani.

04-26
37:53

Zinga: Walioidhinisha ujenzi wa nyumba kwenye njia za mito wachukuliwe hatua, asema Pius Masai Mwachi

Mtaalamu wa majanga Pius Masai Mwachi ametaka serikali kuwachukulia hatua kali, maafisa wa umma ambao waliidhinisha ujenzi wa majengo/nyumba kwenye njia za mito ambazo zimesombwa na kusababisha vifo kutokana na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa humu nchini wakati huu.

04-25
32:38

Zinga: Mwelekeo wa Siasa za chama cha ANC ni Upi ?

Licha ya siasa za muungano wa Kenya Kwanza kwamba vyama tanzu vya muungano huo vivunjiliwe mbali, mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha ANC Kelvin Lunani anasema chama hicho kiko imara na kina mipangilio yake ya siasa, je kitavunjiliwa mbali ?

04-24
49:23

Zinga: Viwango vya mafunzo ya udereva nchini viko chini, Alfayo Otuke

Kulingana na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani Alfayo Otuke, Asilimia 30 ya madereva wako na leseni bandia za kuendesha gari, na kwamba Viwango vya mafunzo ya udereva nchini viko chini.

04-23
51:01

Zinga: Wengi wa waathiriwa wa machafuko ya baada ya Uchaguzi wa 2007 wanahangaika

Kulingana na Leah Aoko kutoka shirika la Utu Wetu ambalo linafanya kazi la kuwashughulikia wahanga wa machafuko ya baada uchaguzi , waathiriwa wengi wanaishi na hofu ya maisha na machungu ya kuwapoteza wapendwa wao, baadhi yao wakingojea kufidiwa.

04-12
49:36

Zinga: Wauguzi hawajagoma, mkuu wa wauguzi Nairobi atoa hakikisho

Mkuu wa wauguzi hapa jijini Nairobi amepuuzilia mbali taarifa kwamba wauguzi wangeungana na madaktari katika kuishinikiza serikali kutimiza matakwa yao. Boaz Onchari amesema hakuna sheria inayosema waungane na madaktari wanapogoma huku akishtumu wanaompiga vita katibu mkuu wa wauguzi Seth Panyako.

04-11
45:25

Zinga: Kuwasherehekea na kuwatambua mashujaa wa Imani

Wakfu wa Heroes and Heroines unatazamia kuwasherehekea wakristu na waumini waliohudumu kwa muda mrefu na ambao kujitolea kwao katika safari ya mahubiri kumegusa maisha ya watu wengi.

04-10
34:18

Zinga: Serikali bado haijajitolea kumaliza mgomo wa madaktari asema Seneta Hamida

Seneta Mteule wa chama cha ODM Hamida Kibwana ameelezea kusikitishwa kwake na kimya cha serikali kuhusiana na mgomo unaendelea wa madaktari. Akizungumza leo na Radio Taifa Seneta Hamida Kibwana amesema serikali inafaa kuchukulia mgomo huu kama swala la dharura kwani wanaoumia zaidi ni Wananchi.

04-04
39:14

Zinga: Hakuna afisa wa trafiki anatumwa kuokota hongo na mkubwa wake kamanda wa trafiki nchini asema

Kamanda katika idara ya trafiki humu nchini amefutilia mbali ripoti kwamba maafisa wa trafiki hutumwa na wakubwa wao kuwaokotea hongo kutoka kwa umma akisema kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua kali

02-07
39:43

Zinga: Je, Kenya imepiga hatua katika kupambana na Ufisadi ?

Katika makala ya leo ya Gumzo Pevu tunangalia swala la Ufisadi na ulaji rushwa, leo hii tunaye Philip Kagucia kutoka tume ya maadili na kupambana na ufisadi, kutuekea bayana tulipo kama taifa.

12-07
43:52

Zinga: Mustakabali wa Mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa ni upi?

Kulingana na Mchambuzi wa masuala ya siasa Javas Bigwambo ripoti iliyowasilishwa na kamati teule ya NADCO kwa Rais Ruto na Kinara wa Upinzani Raila Odinga imewaacha wengi wakihoji mengi kuihusu, huku mipasuko ikishughudiwa katika mrengo wa Upinzani.

12-05
48:43

Zinga: Mwaka mmoja wa Hustler Fund, imekufaidi ?

Waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogo ndogo Simon Chelugui amesema Mfuko wa Hustler Fund umekopesha zaidi ya bilioni 39 kwa wakenya milioni 21 751 elfu

11-28
50:57

Zinga: Kuadhimisha Siku ya watoto duniani

Siku ya watoto Duniani huadhimishwa kila Novemba 20 ikilenga kukuza na kusherehekea ustawi na Haki za Watoto Duniani. Ni kumbukumbu ya kupitishwa kwa Azimio la Haki za Mtoto lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mwaka 1989

11-21
41:50

Zinga: Mageuzi katika idara ya polisi

Idara ya polisi humu nchini kwa muda imefabnyiwa mageuzi huku mapendekezo kadha wa kadha yakitolewa na na majopo teule lengo kuu kuimarisha idara hii, lakini je, kuna mapya katika idara hii ?

11-21
52:22

Zinga: Siasa za mazungumzo ya Taifa na gharama ya maisha

Mbunge wa Funyula Wilberforce Ojiambo amesema serikali ya Kenya Kwanza imeshindwa kushughulikia gharama ya juu ya wakenya huku akimtaka Rais William Ruto kujitokeza kusghulikia hali hiyo.

11-16
45:39

Zinga: Mchakato wa kumtimua Gavana

Wawakilishi wadi wa kaunti ya Meru walipiga kura ya kumwondoa madarakani gavana Kawira Mwangaza kwa tuhuma za mbali mbali miongoni mwao upendeleo pamoja na utumizi mbaya wa mamlaka, lakini Je, ushahidi uliowasilisha leo mbele ya seneti ni tosha kumbandua gavana wa Meru Gavana Mwangaza ?

11-07
47:56

Zinga: Suluhu ya gharama ya maisha ni ipi ?

Ongezeko la gharama za maisha nchini Kenya limekuwa tatizo kubwa kwa raia wake, hasa kutokana na bei zinazoongezeka za bidhaa muhimu. Lakini ni nini kinachoweza kufanywa ili kupunguza mkazo huu wa kiuchumi na kuboresha hali ya maisha kwa raia wa Kenya?

11-06
44:17

Zinga : Mtihani wa Kitaifa wa KCPE watamatika

Mtihani wa kitaifa wa KCPE umefikia tamati hii. Watahiniwa wa mwaka huu ni kundi la mwisho wa mtaalĂ  wa 8.4.4

11-02
31:55

Zinga: Zogo la Wachuuzi Nairobi

Baada ya Kaunti ya Nairobi kupiga marufuku uchuuzi wa bidhaa Katika baadhi ya barabara katikati mwa jiji, Wanasiasa na Makundi mbali mbali wamejitokeza kupinga hatua hii ya Gavana Sakaja ambayo wanasema 'Haijakusudiwa na inakosa kutoa njia mbadala kwa Wachuuzi. Lakini je, ni sawa Wachuuzi wadogo wadogo kuondolewa katikati mwa jiji na barabarani hapa Nairobi?

11-01
44:45

Recommend Channels