09 OKTOBA 2025
Update: 2025-10-09
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya posta Duniani na tunakupeleka nchini Tanzania ambako huko Sabrina Said wa idhaa hii amefuatilia harakati za huduma hiyo kwenye shirika la Posta Tanzania lililoanzishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1993 na kuanza kutoa huduma Januari 1994.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha tangazo la makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka wote huko Gaza lililotolewa na Rais wa Marekani , akiyaita makubaliano hayo ni mafanikio yaliyohitajika sana baada ya miaka ya mzozo..
- Licha ya mzozo unaoendelea na changamoto za miundombinu nchini Sudan, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF leo limesema limefanikiwa kutoa chanjo kwa zaidi ya watoto 740,000 walio chini ya umri wa miaka mitano kati ya Januari na Juni 2025, na kutoa dozi zaidi ya milioni 16.
- Katika Siku ya Posta Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewashukuru wafanyakazi milioni 4.6 wa posta wanaounganisha jamii kote duniani.
- Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "FUNDI HANA CHOMBO"
Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Comments
In Channel