22 OKTOBA 2025
Update: 2025-10-22
Description
Hii leo jaridani tunaangazia mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga, elimu kuhusu uraia nchini Sudan kusini, na kilimo endelevu na vijana nchini Rwanda.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali.
- Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.
- Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Comments
In Channel