Doctor Rafiki Afrika

Habari, Kwa majina naitwa Dr. Julieth Sebba, MD. Ni daktari na mtafiti katika sekta ya afya Tanzania. Ungana nami kila wiki, nikikushirikisha maarifa mbalimbali katika kuboresha afya yako, afya ya familia yako na jamii kiujumla.

NJIA ZA KUKABILIANA NA MAUMIVU YA MGONGO

Habari Rafiki, karibu kwenye episode nyingine ya Doctor Rafiki Africa, na wiki hii tunazungumzia njia za kukabiliana na maumivu ya mgongo. Ni furaha yetu utaenda kujifunza mambo mbalimbali ukiungana na wataalumu wetu wa masuala ya physiotherapy. Karibu kusikiliza

09-11
29:43

Nini kinasababisha maumivu ya mgongo ya mara kwa mara

Je, unakumbwa na maumivu ya mgongo mara kwa mara? Katika video hii, daktari wa mazoezi (physiotherapy) Emmanuel Jacob ndani ya Doctor Rafiki Africa ataeleza kwa undani sababu kuu zinazoweza kusababisha maumivu ya mgongo ya mara kwa mara, dalili unazopaswa kuzingatia, na njia bora za kuzuia na kutibu.

09-04
17:03

Supplements kwa Makundi Maalumu – Fahamu Nini cha Kuzingatia

Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki kwa kushirikiana na Nutrihaven, tunazungumzia umuhimu wa virutubisho kwa makundi maalumu kama wazee, wanawake kabla na baada ya menopause, wajawazito, wanaonyonyesha, na watu wenye magonjwa sugu. Dr. Julieth Sebba na Dr. Carl Mhina wanakupa mwongozo wa kitaalamu kuhusu wakati, sababu, na tahadhari za kutumia virutubisho kwa afya bora.

08-14
32:44

Je, Kila Suppliment Za Kula Ni Salama Kwako?

Chapters (00:00:00) - Foreign Supplements

08-06
34:16

NJIA 05 ZA KUJIANDAA ILI KUPATA MAZIWA YA KUTOSHA BAADA YA KUJIFUNGUA

Habari Rafiki, tukiwa kwenye wiki ya unyonyeshaji karibu tujifunze njia 05 za kujiandaa ili kupata maziwa ya kutosha baada ya kujifungua, tukiwa na mtaalamu wa lishe na unyonyeshaji, Idda Katigula.   Kwa maulizo na ushauri Email: dr.rafikiafrica@gmail.com

07-30
45:56

JE NI SALAMA KUNG'OA JINO KIPINDI CHA UJAUZITO | EP 2

Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki Africa, Dkt. Julieth Sebba anazungumza na Dkt. Evarist Wilson, daktari bingwa wa kinywa na meno, kuhusu usalama wa huduma za meno kwa wajawazito. Usikose kujua ukweli wa kitaalamu kuhusu tiba ya meno wakati wa ujauzito!

07-25
18:37

JE NI SALAMA KUNG'OA JINO WAKATI WA UJAUZITO?

Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki Africa, Dkt. Julieth Sebba anazungumza na Dkt. Evarist Wilson, daktari bingwa wa kinywa na meno, kuhusu usalama wa huduma za meno kwa wajawazito. Usikose kujua ukweli wa kitaalamu kuhusu tiba ya meno wakati wa ujauzito!

07-18
28:26

Fahamu kuhusu Bidhaa salama na zisizo salama za Ngozi

Hi rafiki, mambo vipi? karibu kwenye episode ya leo, na wiki hii tunazungumzia suala zima la ngozi tukiangazia kuhusu bidhaa salama na zisizo salama za ngozi. Karibu ungana nami Dr. Julieth Sebba nikiwa na daktari bingwa wa ngozi Dr. Caroline Masanje.

07-11
24:41

Jinsi ya kutunza ngozi yako usipate chunusi | Dr. Caroline Masanje

Habari Rafiki, karibu kwenye episode mpya ya Doctor Rafiki Afrika, tukienda kuzungumzia suala zima la ngozi. Wiki hii tunaungana na Daktari bingwa wa masuala ya ngozi, Dr. Caroline Masanje tukiangazia jinsi au namna ya kutunza ngozi yako usipate chunusi. Karibu Kusikiliza. Unaweza kutuandikia maswali au maoni yako kupitia: Email: dr.rafikiafrica@gmail.com

06-27
20:53

Njia salama za utunzaji wa ngozi yako | Dr. Rafiki Africa x Dr. Salva Nicas

Karibu kwenye video hii maalum ya Dr. Rafiki Africa tukishirikiana na Dr. Salva, mtaalamu wa magonjwa ya ngozi, ambapo tunazungumzia mbinu salama na bora za kuitunza ngozi yako kila siku. Utajifunza: ✅ Sababu za matatizo ya ngozi yanayotokana na utunzaji usio sahihi ✅ Namna ya kuchagua bidhaa salama kwa ngozi yako ✅ Vidokezo vya asili vya kuimarisha afya ya ngozi ✅ Mambo ya kuzingatia kwa ngozi yenye mafuta, kavu au mchanganyiko

06-14
39:40

Je, ni Kweli kuwa pumu ya ngozi (eczema) haiwezi kupona kabisa?

Habari rafiki, karibu kwenye episode mpya ya leo, tukiendelea na mada yetu kuhusu pumu ya ngozi. Wiki hii tukiwa na Daktari bingwa wa ngozi, Dr. Salva Nicas, tunazungumzia kuhusu suala la kupona kwa pumu ya ngozi (eczema). Je? ni kweli kuwa pumu ya ngozi haiwezi kupona kabisa.   Karibu kusikiliza

06-04
42:00

UNAJUA NINI CHANZO CHA PUMU YA NGOZI (ECZEMA)? KARIBU TUONGEE

Pumu ya ngozi (eczema) ni tatizo linalowaathiri watu wa rika zote, lakini wengi hawajui chanzo chake halisi. Katika kipindi hiki, Doctor Rafiki akiwa na Dr. Salva Nicas, Md, Mmed wanachambua kwa undani visababishi vya pumu ya ngozi, athari zake, na jinsi ya kujikinga au kuitibu. Karibu upate maarifa sahihi yatakayokusaidia wewe na wapendwa wako kuishi maisha bora bila usumbufu wa ngozi. Sikiliza hadi mwisho – afya ni msingi wa maisha!

05-29
36:24

MSIMU WA MAFUA: JINSI YA KUJIKINGA NA KUTIBU

Katika kipindi hiki, Doctor Rafiki anazungumzia ongezeko la mafua katika jamii kipindi hiki cha msimu wa baridi na mvua. Utajifunza visababishi vikuu vya mafua, jinsi yanavyoenea, na hatua rahisi lakini muhimu za kujikinga na kutibu mafua kabla hayajawa makubwa. Sikiliza upate elimu ya afya kwa maisha bora! #doctorrafikiafrica kwa mawasiliano: dr.rafikiafrica@gmail.com

05-14
24:05

KWANINI TUNAWE MIKONO? | DR. RAFIKI AFRICA

Hello Rafiki, karibu kwenye episode nzuri ya Doctor Rafiki Africa, leo tunazungumzia suala zima la 'Kunawa Mikono'. Je ni kweli kunawa mikono kunakulinda na magonjwa? Karibu kujifunza.   Kwa mawasiliano nasi, barua pepe: dr.rafikiafrica@gmail.com

05-06
15:33

Sababu 05 muhimu kwanini mtoto wako apewe chanjo | Dr. Rafiki

Habari Rafiki, Karibu kwenye doctor rafiki podcast, wiki hii tunazungumzia suala zima la chanjo, na tunaenda kukueleza sababu 05 muhimu kwanini mtoto apewe chanjo. Karibu tujifunze pamoja Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia barua pepe dr.rafikiafrica@gmail.com

04-17
11:54

MASWALI 10 JUU YA TB SUGU | DR. RAFIKI AFRICA

Habari rafiki, karibu kwenye dr. rafiki podcast; Karibu ujifuzne kuhusu kifua kikuu sugu, jinsi kinavyoenea, dalili zake, na mbinu za matibabu. Sikiliza majibu ya maswali muhimu kuhusu ugonjwa huu hatari

04-03
18:27

CHANGAMOTO YA HARUFU MBAYA MDOMONI NA UTATUZI WAKE

Habari Rafiki, karibu kwenye doctor rafiki podcast, leo ikiwa ni siku ya afya ya kinywa duniani, tunaangazia suala zima la changamoto ya harufu mbaya mdomoni pamoja na namna ya utatuzi wake. Ungana nami Dr. Julieth Sebba, MD tukiwa na mgeni wetu ambaye yeye ni daktari bingwa afya ya kinywa na meno, Dr. Evarist Wilson.

03-20
24:00

NJIA 05 ZA KUTUNZA UZITO SAHIHI | Doctor Rafiki Africa

Habari Rafiki, Fahamu njia 05 za kutunza uzito sahihi. Karibu ungana nami Doctor Julieth Sebba, MD. 

03-06
25:49

ZIPI CHANGAMOTO NA MABADILIKO BAADA YA MATIBABU YA KANSA

Habari Rafiki, karibu kwenye episode mpya ya doctor rafiki, tukiendelea na mada yetu ya kansa. Wiki hii tunazungumzia kuhusu changamoto na mabadiliko baada ya matibabu ya kansa. Karibu ungana nami host wako Dr. Julieth Sebba, MD.

02-20
21:51

AFYA YA AKILI NA KANSA | HADITHI YA UJASIRI NA TUMAINI

Habari Rafiki, karibu kwenye doctor rafiki wiki hii tukizungumzia ugonjwa wa kansa na jinsi ambayo unaweza kuathiri afya ya akili kwa wagonjwa, familia na hata watoa huduma ya Afya. Fahamu pia hadithi nzuri ya kusisimua ya mwanamke mmoja jasiri aliyejaa na tumaini, tuliyempa jina la 'Amina'.

02-06
17:24

Recommend Channels