26 OKTOBA 2023
Update: 2023-10-26
Description
- Gaza ambako kipindi cha saa 24 cha siku ya 19 ya mapigano kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas kimekuwa kibaya zaidi kwani watu 756 wameuawa Gaza wakiwemo watoto 344 na kufanya idadi ya waliouawa tangu Oktoba 7 kufikia 6,547 kwenye eneo hilo linalokaliwa la wapalestina, imesema Wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni ,WHO lenyewe linawataka Hamas kutoa hakikisho la hali ya mateka wa kiisraeli wanaoshikiliwa na kundi hilo ikiwemo afya zao na iwapo wanapatiwa huduma za msingi.
- Hali ya sintofahamu ikiendelea Gaza, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la nchi wanachama baada ya harakati za kusaka kupitisha maazimio Baraza la Usalama kuhusu mzozo Mashariki ya Kati kugonga mwamba.
- Na kwingineko, hii leo huko Tbilisi, Georgia, shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP na Mfuko wa Tabianchi duniani, GCF wametangaza mradi wa dola milioni 19 utakaotekelezwa mkoani Kigoma nchini Tanzania kwa ajili ya kurejesha mazingira na kujengea mnepo wenyeji na wakimbizi. Mradi utatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Tanzania.
- Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MTEGEMEA NUNDU HAACHI KUNONA.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Comments
In Channel