DiscoverDoctor Rafiki Afrika
Doctor Rafiki Afrika

Doctor Rafiki Afrika

Author: Doctor Rafiki

Subscribed: 78Played: 75
Share

Description

Habari, Kwa majina naitwa Dr. Julieth Sebba, MD. Ni daktari na mtafiti katika sekta ya afya Tanzania. Ungana nami kila wiki, nikikushirikisha maarifa mbalimbali katika kuboresha afya yako, afya ya familia yako na jamii kiujumla.
59 Episodes
Reverse
Habari Rafiki, karibu kwenye episode nyingine ya Doctor Rafiki Africa, na wiki hii tunazungumzia njia za kukabiliana na maumivu ya mgongo. Ni furaha yetu utaenda kujifunza mambo mbalimbali ukiungana na wataalumu wetu wa masuala ya physiotherapy. Karibu kusikiliza
Je, unakumbwa na maumivu ya mgongo mara kwa mara? Katika video hii, daktari wa mazoezi (physiotherapy) Emmanuel Jacob ndani ya Doctor Rafiki Africa ataeleza kwa undani sababu kuu zinazoweza kusababisha maumivu ya mgongo ya mara kwa mara, dalili unazopaswa kuzingatia, na njia bora za kuzuia na kutibu.
Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki kwa kushirikiana na Nutrihaven, tunazungumzia umuhimu wa virutubisho kwa makundi maalumu kama wazee, wanawake kabla na baada ya menopause, wajawazito, wanaonyonyesha, na watu wenye magonjwa sugu. Dr. Julieth Sebba na Dr. Carl Mhina wanakupa mwongozo wa kitaalamu kuhusu wakati, sababu, na tahadhari za kutumia virutubisho kwa afya bora.
Chapters (00:00:00) - Foreign Supplements
Habari Rafiki, tukiwa kwenye wiki ya unyonyeshaji karibu tujifunze njia 05 za kujiandaa ili kupata maziwa ya kutosha baada ya kujifungua, tukiwa na mtaalamu wa lishe na unyonyeshaji, Idda Katigula.   Kwa maulizo na ushauri Email: dr.rafikiafrica@gmail.com
Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki Africa, Dkt. Julieth Sebba anazungumza na Dkt. Evarist Wilson, daktari bingwa wa kinywa na meno, kuhusu usalama wa huduma za meno kwa wajawazito. Usikose kujua ukweli wa kitaalamu kuhusu tiba ya meno wakati wa ujauzito!
Katika kipindi hiki cha Doctor Rafiki Africa, Dkt. Julieth Sebba anazungumza na Dkt. Evarist Wilson, daktari bingwa wa kinywa na meno, kuhusu usalama wa huduma za meno kwa wajawazito. Usikose kujua ukweli wa kitaalamu kuhusu tiba ya meno wakati wa ujauzito!
Hi rafiki, mambo vipi? karibu kwenye episode ya leo, na wiki hii tunazungumzia suala zima la ngozi tukiangazia kuhusu bidhaa salama na zisizo salama za ngozi. Karibu ungana nami Dr. Julieth Sebba nikiwa na daktari bingwa wa ngozi Dr. Caroline Masanje.
Habari Rafiki, karibu kwenye episode mpya ya Doctor Rafiki Afrika, tukienda kuzungumzia suala zima la ngozi. Wiki hii tunaungana na Daktari bingwa wa masuala ya ngozi, Dr. Caroline Masanje tukiangazia jinsi au namna ya kutunza ngozi yako usipate chunusi. Karibu Kusikiliza. Unaweza kutuandikia maswali au maoni yako kupitia: Email: dr.rafikiafrica@gmail.com
Karibu kwenye video hii maalum ya Dr. Rafiki Africa tukishirikiana na Dr. Salva, mtaalamu wa magonjwa ya ngozi, ambapo tunazungumzia mbinu salama na bora za kuitunza ngozi yako kila siku. Utajifunza: ✅ Sababu za matatizo ya ngozi yanayotokana na utunzaji usio sahihi ✅ Namna ya kuchagua bidhaa salama kwa ngozi yako ✅ Vidokezo vya asili vya kuimarisha afya ya ngozi ✅ Mambo ya kuzingatia kwa ngozi yenye mafuta, kavu au mchanganyiko
Habari rafiki, karibu kwenye episode mpya ya leo, tukiendelea na mada yetu kuhusu pumu ya ngozi. Wiki hii tukiwa na Daktari bingwa wa ngozi, Dr. Salva Nicas, tunazungumzia kuhusu suala la kupona kwa pumu ya ngozi (eczema). Je? ni kweli kuwa pumu ya ngozi haiwezi kupona kabisa.   Karibu kusikiliza
Pumu ya ngozi (eczema) ni tatizo linalowaathiri watu wa rika zote, lakini wengi hawajui chanzo chake halisi. Katika kipindi hiki, Doctor Rafiki akiwa na Dr. Salva Nicas, Md, Mmed wanachambua kwa undani visababishi vya pumu ya ngozi, athari zake, na jinsi ya kujikinga au kuitibu. Karibu upate maarifa sahihi yatakayokusaidia wewe na wapendwa wako kuishi maisha bora bila usumbufu wa ngozi. Sikiliza hadi mwisho – afya ni msingi wa maisha!
Katika kipindi hiki, Doctor Rafiki anazungumzia ongezeko la mafua katika jamii kipindi hiki cha msimu wa baridi na mvua. Utajifunza visababishi vikuu vya mafua, jinsi yanavyoenea, na hatua rahisi lakini muhimu za kujikinga na kutibu mafua kabla hayajawa makubwa. Sikiliza upate elimu ya afya kwa maisha bora! #doctorrafikiafrica kwa mawasiliano: dr.rafikiafrica@gmail.com
Hello Rafiki, karibu kwenye episode nzuri ya Doctor Rafiki Africa, leo tunazungumzia suala zima la 'Kunawa Mikono'. Je ni kweli kunawa mikono kunakulinda na magonjwa? Karibu kujifunza.   Kwa mawasiliano nasi, barua pepe: dr.rafikiafrica@gmail.com
Habari Rafiki, Karibu kwenye doctor rafiki podcast, wiki hii tunazungumzia suala zima la chanjo, na tunaenda kukueleza sababu 05 muhimu kwanini mtoto apewe chanjo. Karibu tujifunze pamoja Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia barua pepe dr.rafikiafrica@gmail.com
Habari rafiki, karibu kwenye dr. rafiki podcast; Karibu ujifuzne kuhusu kifua kikuu sugu, jinsi kinavyoenea, dalili zake, na mbinu za matibabu. Sikiliza majibu ya maswali muhimu kuhusu ugonjwa huu hatari
Habari Rafiki, karibu kwenye doctor rafiki podcast, leo ikiwa ni siku ya afya ya kinywa duniani, tunaangazia suala zima la changamoto ya harufu mbaya mdomoni pamoja na namna ya utatuzi wake. Ungana nami Dr. Julieth Sebba, MD tukiwa na mgeni wetu ambaye yeye ni daktari bingwa afya ya kinywa na meno, Dr. Evarist Wilson.
Habari Rafiki, Fahamu njia 05 za kutunza uzito sahihi. Karibu ungana nami Doctor Julieth Sebba, MD. 
Habari Rafiki, karibu kwenye episode mpya ya doctor rafiki, tukiendelea na mada yetu ya kansa. Wiki hii tunazungumzia kuhusu changamoto na mabadiliko baada ya matibabu ya kansa. Karibu ungana nami host wako Dr. Julieth Sebba, MD.
Habari Rafiki, karibu kwenye doctor rafiki wiki hii tukizungumzia ugonjwa wa kansa na jinsi ambayo unaweza kuathiri afya ya akili kwa wagonjwa, familia na hata watoa huduma ya Afya. Fahamu pia hadithi nzuri ya kusisimua ya mwanamke mmoja jasiri aliyejaa na tumaini, tuliyempa jina la 'Amina'.
loading
Comments 
loading