17 NOVEMBA 2025
Update: 2025-11-17
Description
Hii leo jaridani tunaangazia kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ukatili wa kijinsia na zoezi la mahakama tembezi nchini Sudan Kusini.
- Mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari (IRMCT) umeamua kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari, Félicien Kabuga, hana uwezo wa kiafya kusafiri kwenda Rwanda, uamuzi unaositisha mpango wa awali wa kumhamisha kwenda nchini Rwanda ili kuachiwa kwa muda kutokana na hali yake ya kiafya kuwa tete.
- Dunia inajiandaa kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa Novemba hadi tarehe 10 Disemba, kampeni inayolenga kuongeza uelewa na kutoa wito wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote. Na katika kuelekea maadhimisho hayo, Sabrina Saidi ameandaa taarifa kutokea huko nchini Ethiopia, akiangazia simulizi ya mwanamke ambaye ameamua kuvunja mzunguko wa mila zenye madhara kwa jamii yake.
- Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudani Kusini UNMISS wakishirikiana na wizara ya haki na masuala ya katiba nchini humo wanaendeleza zoezi la mahakama tembezi nchini humo, mradi ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Norway ili kuhakikisha wananchi hususan wale walio na kesi mahakama wanapata haki.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Comments
In Channel

















