18 NOVEMBA 2025

18 NOVEMBA 2025

Update: 2025-11-18
Share

Description

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Brazil kwenye mkutano wa COP30, ambako Dkt. Richard Muyungi, Mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania anaeleza ni nini bara la Afrika linahitaji.

  1. Umoja wa Mataifa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio namba 2803 la Baraza la Usalama kuhusu Gaza hapo jana, ukilitaja kuwa hatua muhimu katika kuimarisha usitishaji mapigano. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anazitaka pande zote kuheshimu kikamilifu makubaliano hayo na kutafsiri kasi ya kidiplomasia kuwa hatua za dharura na za wazi kwa watu walioko katika eneo hilo. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Guterres, Stéphane Dujarric, amesema Umoja wa Mataifa umejizatiti kuongeza misaada ya kibinadamu na kuunga mkono jitihada zinazoelekezwa katika hatua inayofuata ya usitishaji mapigano.
  2. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali ya kibinadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini bado ni tete. Mkurugenzi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Kanda ya Afrika Patrick Youssef  ambaye amerejea hivi karibuni kutoka DRC amewaleza waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi kwamba raia wa DRC wanaendelea kubeba mzigo mzito wa mapigano, hata wakati shughuli chache za kibiashara zikiendelea kurejea Goma. Ametoa tahadhari kuwa mgogoro huo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili, ukatili wa kingono unaongezeka, na zaidi ya asilimia 70 ya watu waliojeruhiwa kwa silaha mwaka huu ni raia.
  3. Kuanzia leo tarehe 18 inaanza Wiki ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usugu wa Vijiumbemaradhi dhidi ya dawa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa usugu wa vimelea yaani hali ambapo bakteria, virusi na vijidudu vingine havidhuriki tena kwa dawa tayari unatishia mifumo ya afya, uchumi na uhakika wa chakula. Kwa kaulimbiu “Chukua Hatua Sasa: Linda Leo Yetu, Linda Mustakabali Wetu,” WHO inatoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya, wakulima, wadau wa mazingira na umma kuchukua hatua madhubuti kutekeleza ahadi za kisiasa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi sugu ya dawa.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UPUNGUFU"

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Comments 
00:00
00:00
x

0.5x

0.8x

1.0x

1.25x

1.5x

2.0x

3.0x

Sleep Timer

Off

End of Episode

5 Minutes

10 Minutes

15 Minutes

30 Minutes

45 Minutes

60 Minutes

120 Minutes

18 NOVEMBA 2025

18 NOVEMBA 2025

Leah Mushi