19 NOVEMBA 2025
Update: 2025-11-19
Description
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe katika siku ya Choo Duniani, simulizi za wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan, na usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR).
- Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo.
- Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha.
- Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka.
Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Comments
In Channel

















