Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa
Description
Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na
desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali
inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa.
Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata
tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa
kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu
na kupiga marufuku tendo hilo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa
ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15
hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya.
Katika makala haya tunaangazia namna tamaduni
hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama
hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata
elimu na kuishi bila unyanyasaji.



