ICRC yapambana kutoa huduma za afya za dharura ndani ya saa 96
Description
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC mara nyingi hubidi kuhudumu katika maeneo yenye mizozo kutoa huduma za dharura ,msaada wa kibinadaam ikiwemo afya
Ili kukabiliana na changamoto za kuafikia malengo yake ya kutoa huduma za afya za dharura katika uwanja wa vita ,maeneo yenye majanga ,imebidi kufumbua mbinu ya kuwa na hospitali za muda ambazo zinajengwa kutumia hema na zinaweza kufanya kazi ndani ya saa 96
ICRC inaendelea na mafunzo ya kuwaandaa wahudumu wa afya wanaohudumu katika mazingira hatarishi ,ili wapate kuhudumu ipasavyo
Mafunzo hayo yanatolewa kwenye hospitali halisi ambazo hutumika katika maeneo ya mizozo ,ambapo wahudumu hao hutakiwa kushughulikia mazingira tofauti ya dharura
Mafunzo hayo yamefanyika nchini Kenya mara mbili ambapo wahudumu hao kutoka maeneo tofauti wanawekwa kwenye makundi na kutakiwa kutangamana na kushughulikia dharura tofauti kabla kuanza kutumwa kwenye maeneo ya mizozo