Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika
Description
Kungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa
Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.
Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.
Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF
MSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.