DiscoverSiha Njema
Siha Njema
Claim Ownership

Siha Njema

Author: RFI Kiswahili

Subscribed: 9Played: 111
Share

Description

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

232 Episodes
Reverse
Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito  Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kutoka mataifa matano ya Afrika yanashinikiza uwekezaji kwenye kubainisha ,kuzuia na kutoa huduma kwa akina mama waja wazito. Isitoshe ushirika kwa wanaume kwenye maswala ya uzazi ili wanapokuwa wana ufahamu wanaweza kusaidia kwenye mapambano hayo
Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu. Kurahisisha  safari hiyo kituo cha  Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi ; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo.   Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi, wana ari mpya kupambana na wanaongeza furaha katika maisha yao kutokana na kupata marafiki ambao wanahimizana namna ya kuushinda ugonjwa wa Saratani.
Chanjo mpya za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB zitakuwa tayari kufikia mwaka 2029 Hadi sasa chanjo 16 zimekuwa zikifanyiwa majaribio na ikiwa zitaidhinishwa zitaokoa maisha ya watu zaidi ya milioni saba kufikia 2050 haswa katika mataifa yanayoendelea. Kwa miongo kadhaa chanjo ya pekee ambayo imekuwa ikitumika kuzuia TB ni chanjo ya BCG ambayo mtoto anapewa pindi anapozaliwa. Wanaharakati wanakiri hatua muhimu zimepigwa kupambana na TB ila uwepo wa chanjo itakuwa hatua muhimu katika mapambano hayo.
Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo . Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi  kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus Kundu mkurugenzi wa mamlaka ya kilimo na chakula nchini Kenya anafafanua.
Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona
loading
Comments