Utapiamlo unaweza kukusababishia Diabetes aina ya 5 wameonya watalaam wa afya
Update: 2025-08-26
Description
Hivi karibuni watalaam wa afya pamoja kwa ushirikiano na shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo
Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini.
Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.
Comments
In Channel