MONUSCO imelaani vikali mashambulizi ya ADF Lubero nchini DRC yalioua raia 89
Update: 2025-11-21
Description
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi
Comments
In Channel

















