Siha Njema

<p>Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.</p>

Utengano wa familia unaweza kuleta shinikizo la damu au kisukari

Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo  hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe  na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi. Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au  kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka. Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.

09-02
10:04

Utapiamlo unaweza kukusababishia Diabetes aina ya 5 wameonya watalaam wa afya

Hivi karibuni watalaam wa afya pamoja  kwa ushirikiano na  shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini. Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.

08-26
10:06

Unachohitaji kufahamu kuhusu ugonjwa wa Pneumonia unaoshambulia mapafu yako

Watu wengi hudhani kuwa Pneumonia husababishwa na baridi kuingia kwenye kifua lakini watalaam wanasema chanzo cha Pneumonia ni vimelea kushambulia mapafu na mfumo wa kupumulia Watalaam wa afya wanasema ndani ya wiki moja, mtu aliye na Pneumonia hugundulika kwa kuwa anapata ugumu wa kupumua au hata kukosa hewa.

08-21
09:12

Kwa nini ni muhimu kuongeza uwekezaji bunifu katika afya ya watoto

Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika  imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla. Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu. Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu  wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu. Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo kwa wakati mwingi huwekeza kwenye miradi inayozingatia matakwa yao. Aidha ili kuhakikisha kuwa huduma za afya kama uchomaji chanjo zinawafikia wanajamii wote ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kuimarisha huduma za wahudumu wa afya wa jamii ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawafikia watoto walengwa baadala ya wazazi kupata ugumu wa kwenda kusaka huduma hizo.

08-12
10:14

Watalaam waonya ongezeko la visa vya H pylori katika maeneo ya mijini

H pylori isipotibiwa inaweza kugeuka kuwa saratani ya tumbo ,watalaam wameonya Katika makala haya,tunaangazia  sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kupata maambukizo ya H pylori na matibabu yake. Matibabu yake kwa mujibu wa daktari Alex Mungala anayehudumu jijini Nairobi yanaweza kukabiliwa na usugu wa vimelea ,ni ghali na si rahisi kupatikana katika vituo vya afya vya daraja la kwanza.

08-05
10:03

Ukiwa utatembea hatua elfu saba kila siku unaweka magonjwa hatari mbali

Utafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na  kupoteza kumbu kumbu Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya. Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu. Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi  la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku. Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi. Wapo waliokuwa na wanatumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu na sasa wameachana nazo. Aidha wengine wameeleza matembezi kuwaondolea maumivu ya viungo na pia kupata marafiki wazuri.

07-29
10:06

Watalaam waonya kukaa muda mwingi kunaweza kukusababishia kifo cha mapema

Kukaa kwa zaidi ya saa sita mfululizi kila siku inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya uti wa mgongo,kisukari,shinikizo la damu na kifo cha mapema

07-23
10:09

Baadhi ya hospitali nchini Kenya zinazalisha chakula kuwalisha wagonjwa

Katika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao

07-15
10:30

Serikali ya Kenya yazingatia afya ya akili miongoni wa vikosi vya usalama

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema polisi wenye changamoto za afya ya akili hawatafukuzwa kazi bali watapewa matibabu stahiki Kumeshuhudiwa hivi karibuni visa vya polisi kutumia silaha zao visivyo na utendakazi wao kukosolewa na raia pamoja na wanaharakati wa haki

07-10
09:36

Je ni muda wa nchi za Afrika kujadili huduma ya kusaidiwa kufa ?

Hivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila  kushinikizwa .

07-02
10:12

Sera ya Kenya kuhakikisha raia wake wanafanya mazoezi kila mara

Takwimu zinaonesha watu wengi kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kuishi bila kufanya mazoezi na kula vibaya Sera hii itatoa mwongozo wa  taasisi za serikali na binafsi kuweka mikakati ya kuruhusu mazoezi ya kila mara wakati wa kazi au nje ya kazi

06-25
10:06

Mwili wako unavyowasiliana kupitia utendakazi wake na kukupa onyo kukiwa tatizo

Kila siku mwili wako hukuzungumzia na ni jukumu lako kusoma mwili wako na kuelewa unasema nini au unakuonya kuhusu nini Baadhi ya matatizo ambayo unaweza kujiepusha nayo ni matatizo ya afya ya akili ,kufeli viungo muhimu au mifumo yako ya afya. Na ili kuhakikisha mwili wako unazungumza na kutoa taarifa iliyo sahihi kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kwa mfano kupata muda wa kutosha kulala,kupata lishe bora  na kufanya mazoezi 

06-20
10:08

Uhusiano wa karibu kati ya matatizo ya tezi koo na afya yako ya akili

Matatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa  dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali  kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid  Disease Awareness Kenya Foundation ,TDAK,  Sarah Katulle anaelezea umuhimu wa wagonjwa kuwa kwenye kundi ambapo wanaweza kushirikishana kuhusu mbinu mbadala ya kuishi na matatizo hayo kando na matibabu. Kundi hilo linawasaidia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa ,mahabara maalum na dawa sahihi. Aidha TDAK ili kuwasaidia wagonjwa hao kuishi maisha ya kawaida wakiwa kazini ,inawaandikia barua ambazo zinawasilishwa kwa maajiri kutambua hali halisi ya wagonjwa na mahitaji yao.

06-12
10:00

Mzigo wa uvutaji sigara Misri ulivyo pasua kichwa kwa afya ya wengi

Misri ipo kwenye njia panda  kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta  mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya  serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa  za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi  na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho la pili sheria zake za kutoza ushuru bidhaa za tumbaku iwapo lengo ni kuleta mapato kwa serikali ,kuwafaidi wazalishaji au kwa maslahi ya afya ya wengi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,WHO,  asilimia 20-25% ya watu wazima nchini Misri huvuta sigara.

06-03
09:55

Mipango tofauti ya matibabu ya matatizo ya Tezi koo ambayo hutumika Afrika

Kabla mgonjwa yeyote kuanzishwa kwenye  matibabu, awe ana tatizo la tezi koo kuzalisha homoni kupitiliza au kushindwa kuzalisha, ni sharti vipimo maalum kufanyika Kipimo cha kwanzo ni inaangazia homoni tofauti inayozalishwa na tezi koo na hii mtu yeyote anaweza kufanya katika wakati wa kufanya vipimo kujua hali yake ya afya ,hapa mtu si lazima awe ameonesha dalili za tezi koo kuwa na tatizo.Kipimo cha pili ambacho ni muhimu huzingatia zaidi  viwango vya  homoni tatu muhimu zinazozalishwa na tezi koo ambayo ni  (TSH), thyroxine (T4), na  triiodothyronine (T3) .Matokeo yataamua ni mpango gani wa matibabu mgonjwa atapewa  dawa,kudhibiti homoni au kuzalisha homoni mbadala tezi koo inaposhindza kazi yake.Kando na dawa kama mpango wa matibabu ,wagonjwa wenye uvimbe wanaweza kushauriwa kufanya upasuaji kuondoa tezi koo ,sehemu yake au yote.Kuna pia mpango wa kutumia mianzi na madini ya Iodine maarufu kama Radioiodine mpango ambao ni sharti kufanywa kwa ueledi mkubwa na kwenye vituo vya afya vilivyo na vifaa vya viwango vya juu.

05-28
10:06

Matatizo ya tezi ya koo ambayo yanaweza kukusababishia matatizo ya akili

 Matatizo ya tezi ya koo ,kwa kawaida  yananaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland).  Homoni inapokuwa kidogo hali ambayo inafahamika kama Hypothyroidism, hii inaashiria kwamba tezi inafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo .Mtu aliye na hali hii ,anakuwa hana nguvu ,nywele kudondoka  na hata mzunguko wake wa mwezi wa damu huvurugika.Madini hayo yanapokuwa mengi inamanisha tezi inafanya kazi kupitliza kuzalisha homoni iliyozidi  kwenye mzunguko wa damu na kuchanganyika na vitu vingene ambavyo husababisha kutengeneza kama sumu fulani ambayo huchoma mafuta yaliyo kwenye hifadhi mwilini, mishipa ya fahamu huathirika kiasi kidogo.Mtu ambaye ameathiriwa na aina hii ya pili, huanza kupunga uzito na umbo la mwili taratibu baadaye madhara yanapoongezeka mtu anaanza kupoteza kumbukumbu, anakuwa na hasira, anakula sana, nywele zinanyonyoka mpaka anapata upara, magoti yanakosa nguvu na mtu anashindwa kutembea.Moyo kwenda mbio , macho yanavimba sehemu ya juu kope na jicho lenyewe linatoka nje kama vile linadondoka.Ni vizuri kuwahi hosipitali ili kupata vipimo ambavyo vinaangazia utendakazi wa tezi ,kwa jina la kiingereza ,Thyroid Function ,ili kubaini iwapo una tatizo la kwanzo au la pili.Na si lazima mtu kuwa na uvimbe ili kubainika kuwa ana tatizo la tezi koo. Kuna wale ambao uvimbe unakuwa upande wa ndani ,wale wenye uvimbe unaonokena nje ya koo ya wale ambao hawana uvimbe wowote.

05-20
10:09

Mfano wa Misri wa kupambana na Malaria unaweza kutumika na mataifa ya Afrika

Misri imepambana kwa karibu miaka 100 kabla kupata cheti cha WHO cha kufaulu kutokomeza Malaria Oktoba 2024 Katika mkakati ambao umetumia Misri kuangamiza Malaria ni udhibiti wa Mbu,ambapo serikali iliwekeza kwenye kupiga dawa kwenye maeneo yanayoweza kuwa makazi ya mbu .Ufuatiliaji na ubainishaji wa haraka  umechangia pia pakubwa kuushinda ugonjwa wa Malaria ,mkakati ambao pia jamii ilibidi kushirikishwa.Kitengo cha afya ya umma kimekuwa kikifanya hamasisho kwa wanajamii kukumbatia mbinu za kuzuia mbu kwa kutumia vyandarua na pia kupata matibabu ya haraka mtu anapoonesha dalili za Malaria.

05-13
09:50

Mchango wa wanaveterinari ulivyo muhimu katika mapambano ya magonjwa ya milipuko

Ongezeko la magonjwa ya milipuko linaibua swala la kwa nini watalaam wa wanyama hawahusishwi kikamilifu katika mifumo ya afya ya binadaam Mpango wa one Health Approach unaonadiwa kwa sasa kwa mataifa ,unahimiza kuipa kipau mbele afya ya wanyama ,ili kuchangia siha njema ,usalama wa chakula na maendeleo endelevu .

05-03
10:07

Kwa nini ni muhimu kuyachunguza maziwa unayotumia nyumbani kulinda afya yako

Kumekuwa na malalamishi ya maziwa yaliyo kwenye soko kusababisha madhara ya kiafya Watalaam wa afya ,bodi inayosimamia bidhaa za maziwa nchini Kenya na wanavetirinari wanasema matatizo hayo huenda yanatokana na uzembe wakati wa uchakataji maziwa ,uhifadhi na pia wafanyabiashara wenye pupa.

05-03
10:00

Changamoto zinazowakumba watalaam wanaojikita kwenye tiba asilia nchini DRC

Baadhi ya changamoto zinazokumba sekta ya tiba asilia ni mwitiko na  ukosefu wa sheria za kuisimamia katika  nchi mbali mbali

04-08
10:00

Recommend Channels